Mi’raaj Imetokea Katika Rajab Na Tarehe Gani Na ‘Ibaada Zipi Za Kutenda?
Alhidaaya.com [2]
SWALI:
Asalam alykum
Miraji imetokea siku gani? Na ibada gani za kutenda katika mwezi huo? Tunaomba mtufutu enyi mashekhe wetu.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kuhusu Mi'iraaj, watu wanafunga na kufanya mambo mengine mambo ambayo hayana dalili wala msingi katika Dini yetu tukufu. Tukio hilo ambalo lilitokea katika maisha ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bila shaka yoyote. Lakini wana Historia wametofautiana kuhusu tarehe na haijulikani kihakika ni gani japokuwa wengine wamechukua ni 27 Rajab, na wengine wametaja miezi na tarehe tofauti na hiyo. Wakati huo hata Swawm yenyewe ilikuwa haijafaradhishwa kwa Waislam. Wala hakuna ‘ibaada yoyote iliyothibiti kutendwa katika mwezi huu isipokuwa tu Rajab ni miongoni mwa miezi mitukufu basi linalopasa ni kukithirisha ‘amali njema na kila aina za ‘ibaadah kujichumia thawabu nyingi.
Kwa maelezo zaidi na faida bonyeza viungo vifuatavyo:
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/38
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7963
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8990
[5] http://www.alhidaaya.com/sw/node/1780
[6] http://www.alhidaaya.com/sw/node/465
[7] http://www.alhidaaya.com/sw/node/137
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9072&title=Rajab%3A%20Mi%E2%80%99raaj%20Imetokea%20Katika%20Rajab%3F%20Na%20Tarehe%20Gani%3F%20Na%20%E2%80%98Ibaada%20Zipi%20Za%20Kutenda%3F