Rajab: Hakuna ‘Ibaadah Maalumu, Swawm, Wala Du’aa Makhsusi Kwa Ajili Ya Mwezi Wa Rajab

 

 

Rajab: Hakuna ‘Ibaadah Maalumu, Swawm,

Wala Du’aa Makhsusi Kwa Ajili Ya Mwezi Wa Rajab

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Assalamu aleikum

Eti kuna lolote la ibada kutekelezwa za mwezi wa Rajab? Watu wanafunga mwezi mzima na wengine wanafunga siku ya Miraji na je kuna dua zake?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

Hakuna uthibitisho wowote wa kuhusiana na ‘ibaadah au Swawm au Swalaah, au du’aa maalumu ya mwezi wa Rajab.  Bali utukufu wake ni utukufu kwa ujumla uliotajwa katika miezi minne mitukufu ambayo humo haipasi kufanya maasi bali inapaswa kutenda mema kwa wingi.

 

Kwa faida zaidi, bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Swawm Katika Mwezi Wa Rajab - Kufunga Mwezi Mzima Au Siku Maalumu Ni Sunnah?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Du’aa Makhsusi Ya Mwezi Wa Rajab Sha’baan na Ramadhwaan Imethibiti?

 

Imaam Ibn Baaz-Kuhusisha Mwezi Wa Rajab Kwa ‘Ibaadah

 

Shaykh Fawzaan: Kuomba: Ee Allaah! Tubarikie Rajab Na Sha´baan Na Tufikishe Ramadhwaan Ni Swahiyh?

 

Uzushi Wa Kuomba Maghfirah Katika Mwezi Wa Rajab

 

Mwezi Wa Rajab: Fadhila Zake Na Yaliyozuliwa Ndani Yake

 

'Amali Za Kutenda Na Mambo Ya Kujiepusha Nayo Katika Miezi Mitukufu

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share