Skip navigation.
Home kabah

Kuchangia Na Kushiriki Shughuli Za Bid-ah Ni Dhambi?

SWALI

Assalaam Alaykum

Nimepatwa na mtihani, mzazi wangu kafariki na ndugu wanataka tusome dua ya hitima mwezi huu, Sasa nauliza je nitoe mchango katika hiyo shughuli?

Pili je kama sitatoa pesa nikahudhuria naweza kula nyama iliyochinjwa katika hitima hiyo, Naomba mnipatie jibu mapema ili niwape msimamo kwani nahofia wasione nimewasaliti ila nataka kama haiwezekaniki niwakatalia kwa points

Wabilah Tawfiq


 



JIBU 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Katika Swali hilo kuna mas-ala mawili ambayo yote hayafai kutendeka; Khitmah na kuchinja kwa ajili ya marehemu:

Khitmah ni jambo la bid'aa (uzushi) kwani halimo kabisa katika mafunzo ya Sunnah, kwa maana hakuna dalili yoyote kama Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya khitma au kukubali ifanywe. Na lau kama ni jambo sahihi basi tungelipata uthibitisho kuwa lilitendeka walipofariki watu wake au Maswahaba    zake. Lakini hakuna hata usimulizi mmoja unaoelezea kuwa lilitendekea zama hizo wala zama za wema waliopita. Hivyo hatuna budi kujiepusha nalo kwani maonyo mengi tumepata kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kujiepusha na mambo ya bid'aa (uzushi).

 

Jambo hili linapomtokea mtu au watu katika jamii wasiopenda kutambua yaliyo sahihi bali kuendeleza mafunzo yasiyo na dalili, huwa ni gumu sana kuliacha. Ni wajibu wetu kuendelea kuwafunza watu na kuwafahamisha mafunzo sahihi tusichoke, hata kama ni jamaa zetu tujitahidi kuwapa nasaha na kutowatenga.

Bonyeza hapa upate maelezo kamili kuhusu hukmu ya Khitmah na ujaribu kuwafikishia ndugu zako ujumbe huo ili wajiepushe nalo.

KHITMA: Kutokufaa Na Madhara Yake

Kuchinja pia kwa ajili ya marehemu, hakuna ushahidi kuwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya hivyo kwa ajili ya mtu aliyekufa ila alichinja kwa ajili ya Umma huu wa Kiislamu katika ibada zinazotendekea siku za Hijjah na pia kwa ajili ya ‘Aqiyqah wanayofanyiwa watoto. Kama alivyowafanyia wajukuu zake kina Al-Hasan na Al-Husayn (radhiya Allaahu ‘anhuma).

Kuchangia katika mambo hayo haifasi kabisa kwani utahesabika kuwa ni mmojawapo wa mwenye kutenda ibada hiyo ya uzushi.

Hivyo inakupasa kwanza ujiepushe kabisa na mambo hayo. Kisha ujaribu kuzuia ibada hizo zisitendeke, na kufanya hivyo utakuwa umetimiza wajibu wako wa kuzuia maovu yasitendeke kama tulivyoamrishwa katika Hadiyth ifuatayo:  

 

عن أَبي سعيدٍ الخُدْريِّ رضي اللَّه عنه قال : سمِعْتُ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ : ((مَنْ رَأَى مِنْكُم مُنْكراً فَلْيغيِّرْهُ بِيَدهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطعْ فبِلِسَانِهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلبهِ وَذَلَكَ أَضْعَفُ الإِيمانِ)) رواه مسلم .

Kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudhriy (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   akisema:

((Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu akiondoe (abadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani)) [Imesimuliwa na Muslim]

Yanayompasa kumfanyia marehemu kama yalivyokuja katika mafunzo ya Sunnah ni; kumuombea du'aa, kumtolea sadaka,  kumfanyia Hajj ikiwa hakuwahi kufanya.  Kwa hiyo badala ya kufanya jambo lisilo na msingi ni bora kufanya yale ambayo hayana shaka yaliyopatikana dalili zake katika mafunzo ya Sunnah. Hivyo vile vile utakuwa umetoa mafunzo sahihi ya Sunnah na utajichumia thawabu kwa hayo.

Bonyeza hapa upate maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya: 

 Kumsomea Khitmah Maiti Kumchinjia Na Kumuombea D'uaa Kwa Pamoja

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Azidi kutuongoza kufuata yaliyo haki na kuacha yaliyo batili.

 

Na Allah Anajua zaidi

 

ASLAAM ALAYKUM Ninaomba

ASLAAM ALAYKUM

Ninaomba msaada wenu juu ya suala ambalo linaniumisha kichwa watu wakilisema na kama utapata nafasi nifafanulia kwa hadith na ushahidi wa Aya juu kutokuwepo kwa hili jambo ama kuwepo kwake.

Suala ni pale mtu anapooa siku ya kwanza tu kumuingilia mke wake ktk tendo la ndoa, Je? kuna ulazima kwa wazee au familia ya upande wa mwanamme kujua kama yule mtoto aliyeolewa na mtoto wao ni bikira ama si bikira, kwasababu haya masuala yapo mpaka leo, na wazee wanasema waoneshwe kitambaa maalum ambacho ni cheupe kama ni ushahidi wa mtoto wa kike kama hajawahi kuingiliwa.

Ahsanteni sana.
Masoud.

ASLAAM ALAYKUM Naomba

ASLAAM ALAYKUM

Naomba kufahamishwa kutuma suala langu ktk mtandao huu waalhidaaya.

Shukrani

Asslaamu

Asslaamu 'alaykum

Tafadhalini tumeni maswali yenu kupitia maswali@alhidaaya.com . Hapa ni mahali pa KUWEKA MAONI TU KUHUSU MAKALA HII.

Jazaakumu Allaahu Khayra

assalam alykum sisi kawaida

assalam alykum
sisi kawaida huwa tunakusanyika pamoja siku moja kwa kila mwezi na kuswali kuleta adhkar na kuomba dua ya pamoja ambazo zimo katika quran na suna sahihi za mtume (s.w)je mambo kama haya yanakubalika?

Asslaamu

Asslaamu 'alaykum

Tafadhalini tumeni maswali yenu kupitia maswali@alhidaaya.com . Hapa ni mahali pa KUWEKA MAONI TU KUHUSU MAKALA HII.

Jazaakumu Allaahu Khayra