Khitmah Kutokufaa Na Madhara Yake
Muhammad Baawazir
Khitmah Ni Nini?
Khitmah kilugha ni kuihitimisha Qur-aan nzima; kuisoma Qur-aan kuanzia mwanzo wake sura namba moja yaani Suratul Faatihah (Alhamdu) hadi mwisho wake ambayo ni sura namba 114 yaani Suratun Naas (Qul A'udhu birabbin Naas).
Lakini imegeuzwa maana hiyo ya kilugha na kugeuka katika matumizi ya walioanzisha huo utaratibu wa kumsomea Maiti Qur-aan na kuita kisomo hicho cha kumsomea Maiti kuwa ni Khitmah kwa sababu ndani yake kuna kuisoma Qur-aan yote. Hukusanyana watu pahala; kwenye nyumba ya marehemu, au ukumbi wa kukodiwa au msikitini na kugawana juzuu kila mmoja na husomwa hiyo Qur-aan kwa sauti na kila mmoja kwa utaratibu wake na bila hata kumalizika. Pia huchomwa ubani n.k. Na wasomao hutaraji thawabu ya kusoma kwao hiyo Qur-aan imfikie Maiti. Na mambo haya yalianza baada ya kupita vipindi kitukufu cha vizazi vitatu ambavyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivisifu.
Baada ya taarifu hiyo, maswali yafuatayo yanamiminika:
1) Watu wanaposoma Khitmah husoma Qur-aan na kusoma Qur-aan ni jambo zuri na la ibada, sasa kwa nini isifae kuisoma kwenye Khitmah?
2) Je, thawabu ya kusoma Qur-aan inamfikia Maiti?
3) Je, hayo yalifanywa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au Makhalifa wake waongofu au hata Maswahaba zake watukufu?
4) Madhara gani yanapatikana kwa kumsomea Qur-aan maiti?
5) Na
Haya ni maswali ambayo nimeyakusanya kwa ufupi kutoka kwa ndugu zetu waliouliza. Na nitajaribu kulijibu moja baada ya jingine kwa kadiri nitakavyowafikishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
1- Je kusoma Qur-aan sio ibada na jambo zuri? Kwa nini isifae kusoma Qur-aan kwenye Khitmah wakati Qur-aan ni du'aa?
Bila shaka taratibu zote za dini yetu zinatoka katika Qur-aan na Sunnah za kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na mipangilio yote ya kiibada na Shari’ah kaishatufundisha yeye na katuwekea mipangilio
Kwa sababu hakuna popote pale kwa ushahidi sahihi panapothibitisha kusoma Qur-aan kwa Maiti, basi jambo
Pia usomaji huo unaosomwa katika Khitmah ni wa kelele na vurugu, kila mmoja husoma ki-aina yake na kwa kelele na wengi hawajui hata hukmu za tajwid. Na ingawa wanadai kuwa wanasoma Qur-aan kisha husoma na dua, Ukweli kusoma Qur-aan ni jambo zuri tena Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth iliyopo kwenye Al-Bukhaariy na imesimuliwa na Abu Muusa Al-Ash’ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) anasema: “Mfano wa yule Muislam asomaye Qur-aan ni kama Utrujjah (tunda lenye harufu nzuri), harufu yake nzuri na ladha yake tamu. Na Muislam asiyesoma Qur-aan ni
Hadiyth hii hata hivyo haikuja kwa kuwasomea Maiti Qur-aan bali ni kuisoma kila wakati na kuonyesha umuhimu wa kuisoma Qur-aan kwa waumini. Na Qur-aan hiyo hiyo ikisomwa nyakati nyingine huenda ikampatia msomaji dhambi badala ya thawabu! Mfano mtu akaisoma Qur-aan chooni, au akiisoma kwa kutaka kumlogea mtu n.k.
Na pia kuisoma kwa Maiti kwa sababu ni jambo la uzushi basi hupelekea katika madhambi na hata motoni kutokana na Hadiyth ya Mtume katika riwaya nyingine aliposema:
"Kila bid'ah ni upotofu na kila upotofu ni motoni" (Mwenyeezi Mungu atuepushe na
Na Mwenyeezi Mungu Anasema:
{{Na isomwapo Qur-aan, isikilizeni, nyamazeni ili mpate kurehemewa}} Al-A’araaf 7: 204.
Na kwenye Khitmah kila mmoja husoma kivyake na juzuu yake kwa sauti na hakuna mwenye kusikiliza.
Na anasema tena Mwenyeezi Mungu katika kuonyesha kuwa Yeye haihataji kuombwa kwa zogo na vurugu kwani Anajua akitakacho mja bila kupiga kelele na mayowe; Anasema:
{{Na mtaje Mola wako kwa UNYENYEKEVU na khofu BILA KUPIGA KELELE katika kauli...}} Al-A’araaf 7: 205
Na wanasema kuwa wao wanamkumbuka Mola wao na kumuomba, hata
2- Je, Thawabu Ya Kusoma Qur-Aan Humfikia Maiti?
Naye Imam An-Nawawiy katika kufafanua kitabu cha Hadiyth cha Imaam Muslim, kwenye Hadiyth hiyo akasema: “Ama kusoma Qur-aan na kukusudia thawabu za kisomo chake kimwendee maiti, na kuswali ili thawabu zake zimfikie na mfano wa haya, amesema Imam Shaafi’iy na Jamhuur ya Wanachuoni (yaani Wanachuoni wengi) kwamba haya hayamfikii maiti”
Imam Ash-Shaafi’y alipoulizwa kuhusu
Na pia akatoa ushahidi wa Hadiyth:
“Anapokufa mwanaadam hukatika amali zake ila kwa mambo matatu...” Taz. kitabu chake maarufu Al-Umm Juzuu ya 4,
Pia katika kitabu maarufu cha madhehebu ya Ki-Shaafi’iy kiitwacho Al-Minhaaj, katika ufafanuzi uliofanywa na Ibnu Nahwy ni kwamba: “Hazimfikii maiti katika madhehebu yetu thawabu za kisomo katika kauli mashuhuri.”
Aliulizwa Shaykh Al-‘Izz bin 'Abdis-Salaam, Mwanachuoni mkubwa wa Misr katika zama zake
“Thawabu za kisomo huzipata msomaji wala hazifiki kwa mwengine” Taz. kitabu cha Hukmu Qiraat Lil Amwaat
Katika kitabu cha As-Sunanu wal Mubtada’aat
"Na kisomo cha Khitmah ambazo wanazozifanyia watu waliokufa na kukusanyika kwenye Khitmah hizo kwa kisomo, na kutawanyiana Juzuu... kutoka katika Msahafu kisha wanaanza kisomo na kumaliza kwa pamoja kwa kitambo kidogo tu kisha hupeleka hidaya thawabu walizozisoma kwa Maiti, ni BID'AH yenye upotofu, mfanyaji wake yuko kwenye upeo wa ujinga."
Naye Mwanachuoni mkubwa maarufu wa Tafsiri ya Qur-aan, Imam Ibn Kathiyr katika Tafsiri ya Suratun Najm Aayah ya 39 ameeleza kutokufaa kusoma Qur-aan na kufika thawabu zake kwa maiti.
Ni wanachuoni wengi maarufu wa kale wa Ki-Shafi’iy waliopinga jambo hilo na sitoweza kuwataja wote waliyoyasema bali nitawataja baadhi yao tu kama wanafunzi wakubwa wa Imaam Ash-Shaafi’iy, Al-Muzaniy, Abu Ishaaq Ash-Shiraziy na wengine wengi. Ukiachilia mbali msururu wa mamia ya Wanachuoni wa madhehebu nyingine na wale ambao hawajifungamanishi na madhehebu yoyote.
3- Je, Hayo Yalifanywa Na Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Au Makhalifa Wake Waongofu Au Hata Maswahaba Zake Watukufu?
Hakuna ushahidi wowote wala Hadiyth yoyote sahihi au hata dhaifu inayoonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kusoma Khitmah au kuwaambia watu wakusanyane na wamsomee maiti wao Qur-aan. Zipo Hadiyth dhaifu na za kutungwa (ma’udhuu) zinasema kuwa maiti asomewe Surat Yaasin au Suratul Faatihah au Ikhlaass (Qul Huwa Allaahu Ahad) mara kumi na moja makaburini!
Hivyo basi, hakuna ushahidi popote pale kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala Makhalifa wake waongofu au hata Maswahaba kwamba walifanya Khitmah.
Kuna baadhi ya watu wa Khitmah wanaodai kuwa wakati ule Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akifiwa na watu wake au marafiki zake na Maswahaba kwa ujumla; kuwa Qur-aan ilikuwa haijashuka yote na hivyo asingeweza kufanya Khitmah. Dai la namna hii ni dai potofu kwa sababu nyingi, baadhi yake ni kuwa; huko ni kumfanya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa hakuwa na maarifa kamili ya dini hii, na kwamba kuna mambo muhimu ya dini yetu aliyoyaacha na hakutufikishia (Mwenyeezi Mungu Atuepushe na dhana kama hizo).
Jibu lingine ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifiwa na binti yake Ummu Kulthuum katika mwaka wa sita, na hapo Qur-aan ilikuwa imeshuka taqriban yote; sasa kwanini Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asimsomee huyo mwanawe mtukufu kama jambo hilo lina manufaa kwa maiti?
Na hata alipokufa yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vipenzi vyake
4- Madhara Gani Yanapatikana Kwa Kumsomea Qur-Aan Maiti?
Madhara makubwa
Mtume amekemea
Anasema katika Hadiyth aliyopokea mama wa Waumini, ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha):
“Mwenye kuanzisha jambo katika dini yetu hii, ambalo halimo, hurejeshewa nalo (halikubaliki mbele ya Allaah)” Al-Bukhaariy, 2697
Nyingine:
“Mwenye kufanya jambo ambalo halimo katika dini (Shari’ah) yetu, basi huwa linamrejelea mwenyewe” Muslim, 1718
Nyingine tushaitaja huko mwanzo nayo:
“Nawausieni Ucha Mungu na usikivu na utiifu hata kama akiwa kiongozi wenu ni mtumwa (katika riwaya nyingine mtumwa mhabashi), na hakika atakayeishi baada yangu ataona khitilafu (tofauti)nyingi, basi (mtakapoona hali hiyo ya uzushi na ghasia katika dini) shikamaneni na Sunnah (mwenendo) wangu, na Sunnah (mwenendo) wa Makhalifa wangu waongofu, na mzibane kwa magego (mzikamate kisawasawa). Na tahadharini na uzushi, hakika kila uzushi ni bid'ah na kila bid'ah ni upotevu” Abu Daawuud 4607 na At-Tirmidhiy 2676 katika riwaya nyingine 'kila upotevu ni kwenye moto (wa Jahannam)'
Nyingine:
“...Uzuri wa maongezi ni maongezi ya Kitabu cha Allaah, Na ubora wa uongofu ni uongofu ulioletwa na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na uovu wa mambo ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu” Muslim, 425
Na Hadiyth ziko nyingi
Na pia Hadiyth nyingine na maneno ya Wanachuoni yanatuonyesha ni jinsi gani kuna umuhimu na ubora wa kukamatana na kushikamanana na SUNNAH za Mtume wetu mpenzi (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwa kila tunavyokamata Sunnah au kuzihuisha (kuzifufua) ndipo ujira wetu na kheri zinavyoongezeka. Na kukamatana na Bid'ah kunakimbiza kheri baraka na kueneza ufisadi na maasi katika jamii. Na ni bora kutosheka na Sunnah chache kuliko kukamatana na bid'ah nyingi.
Mwisho tuangalie kipengele cha tano chenye kuuliza:
5- Na Kama Haifai Basi Ni Jambo Gani Linalofaa Kufanyiwa Maiti Na Litakalomsaidia?
Hadiyth maarufu
Imaam An-Nawawiy anasema katika kitabu chake cha Al-Adhkaar
“Wamekubaliana Wanachuoni kwamba du’aa za kumwombea maiti zinawanufaisha na zinafika thawabu za du’aa hiyo. Na wametoa hoja na dalili ya kauli yake Allaah aliposema:
{{Na waliokuja baada
“Na nyinginezo miongoni mwa Aayah mashuhuri zenye maana kama hiyo; na katika Hadiyth nyingi zilizo mashuhuri
“Ee Mola wangu! Wasamehe watu wa Baqi’i Alghardaq”
na pia aliposema:
“Ee Mola wangu! Wasamehe walio hai wetu na waliokufa wetu” na Hadiyth nyinginezo"
Mwisho wa maneno ya Imam An-Nawawiy.
Pia Maulamaa wanaonelea kuwa miongoni mwa sadaka ni kumfanyia maiti ‘Umrah au Hajj ikiwa alikuwa hajafanya kwa ushahidi huu:
“Mwanamke wa kabila la Juhaynah alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mama yangu alikuwa na nadhiri ya kufanya Haji je, naweza kumlipia (kumhijia)? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamjibu: “Mhijie. Je, mama yako angekuwa na deni usingemlipia? Basi, deni la Mola wako ni bora zaidi kulilipa” Al-Bukhaariy
Na vilevile wanaonelea kuwa mtu anaweza kumfungia maiti yake Swawm ya nadhiri au aliyokuwa anadaiwa hajailipa kwa ushahidi huu:
“Alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ee Mjumbe wa Allaah! Mama yangu amefariki na alipaswa kufunga Swawm ya mwezi mmoja (aliyokuwa akidaiwa) Je, naweza kumfungia? Mtume akajibu kwa kuitikia kisha akamwambia: “Deni la Allaah linastahiki zaidi kulipwa” Al-Bukhaariy
Wengine wanaonelea kuwa yafaa hata kumlipia zile Swawm za deni
Haya ni mambo ambayo ni bora kuyafanya na yana ushahidi sahihi na ndio bora Waislam wakayafanyia kazi zaidi kwani ndio yenye manufaa kwa wenzetu waliotangulia.
Namalizia hapa kwa kuwanasihi ndugu zangu turejee katika njia sahihi na mafundisho sahihi ya mtukufu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na tuyaache yenye mashaka na yenye kutusababishia madhara katika dini yetu.
Mwisho namwomba Allaah Atuongoze wote sisi katika njia iliyonyooka na atusamehe tuliyoyafanya bila elimu au kwa kurithi wazee na Masheikh wetu bila ya dalili, na Atujaalie ni wenye kusikiza maneno na kufuata yaliyo mema.
Wa Allaahu A’alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Assalam Alaykum
Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
MashaAllah makala muhimu sana kwa zama kama hizi ambapo uzushi wa Khitmah umefanywa kama ibadah miongoni ibadah muhimu.
Nagusia hapa kwa kukumbusha ndugu zangu waislamu wenye kasumba hii ya kufanya khitmah, tuache uzushi kama huyu kwani bidah ni miongoni mwa al-kabaair (Madhambi Makubwa). Na tufanye ibadah zetu kwa ufahamu na kama walivyokuwa wakifanya Salafi Swaaleh (Wema waliotangulia)
Shukran sana sheikh wangu baawazir kwa mafunzo haya makubwa, Allah akulipe kila la kheri na akupe afya njema na kukuzidishia nguvu za kuweza kutufunza dini yetu kwa ufahamu mzuri wa qura'n na sunnah zilizosubutu.
Jazakallahu Kheir na Allah Atuongoze sote kwenye Siratwal Mustaqim.