Kuna Hukmu Msichana Ameolewa Na Hakukutwa Na Bikra?

SWALI:

 

Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhaana waala Taala, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu

 

 

Je kuna hukumu yeyote inayohusu kama msichana ameolewa na hakukutwa na bikra.

 

Natanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu Subhaana wa Taala na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

 

Shukurani kwa swali kuhusu ubikira wa msichana anapoolewa.

Suala la ubikira ni suala lenye utata mkubwa sana kwenye jamii zetu kwa kiasi ambacho wenye kuoa huwa wakitazama kama wake zao watatoka damu wanapoingiliwa. Na hili si jambo la lazima kwani ni kawaida kwa msichana kutoka damu anapoingiliwa kwa mara ya kwanza lakini wengine wako nje ya ada hii; kwa maana kuwa hawatoki damu wanapoingiliwa kwa mara ya kwanza. Pia wapo wengine wanaopoteza ubikira wao kwa sababu ya kucheza michezo yenye kuwafanya warukeruke au upandaji wa wanyama, na pia uendeshaji baiskeli pia huwezi kumuondoshea msichana ubikira wake kwani ubikira huondoka kwa kukatika kizinda.

 

 

‘Alaa kulli haal, yatakiwa ikiwa mume ameoa na akaona kuwa mkewe si bikira na hali aliuliza au alijulishwa kuwa mwanamke anayo bikira, basi anaweza kuzungumza naye kutaka kujua ukweli wa kupoteza kwake ubikira na anapaswa kumwamini analolisema. Vinginevyo anaweza kuamua kukataa kuishi naye kwa sababu anaona atakuwa na wasiwasi kila jjmara kwa kumshuku mkewe. Kwa njia hiyo itabidi mume arudishiwe mahari yake.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kumsubiri Bibi Harusi Nje Ya Mlango Kujua Kama Ni Bikra (Kijibu Harusi)

 

 

Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?

 

Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu

 

Vipi Atahakikisha Kama Msichana Anayetaka Kufunga Naye Ndoa Ni Bikra; Na Kama Si Bikra Atajua Vipi?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share