Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?

 

Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaamu Alaykum Nashukuru Sana Kwa Kuweza Kusaidiana Sisi Waislam Wenyewe Kwa Wenyewe Allaah Atuzidishie Mie Nilikuwa Langu Naomba Mnijibu. Je Wanawake Wanaofanya Punyeto Bikira Yao Inaweza Kutoka. Asanteni Sana Kwa Kutuelimisha Allaah Wazidishie Amiiin

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Ubikira au ule ugozi ambao Kiswahili inaitwa kizinda, ni ngozi nyembamba sana ambayo hukatika kwa kutumiliwa nguvu.

 

 

Kujichua ni mojawapo ya njia ambayo inaweza kumfanya msichana akose ubikira wake. Mbali na kuwa kujichua ni haramu katika Dini yetu ya Uislamu. Allaah Aliyetukuka Anasema:

 

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾

Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.Lakini atakayetaka kinyume ya hayo; basi hao ndio wapindukao mipaka. [Al-Mu’minuun: 5 – 7]. Na makusudio mojawapo ya ‘anayetaka kinyume cha haya...’ ni kujichua.

 

 

Soma zaidi kuhusu masuala ya kujichua:

 

Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?

 

Kutumia Kitu Kujitoa Matamanio Nini Hukmu Yake

 

Mwanamke Kujichezea Hadi Apate Matamanio Afanye Ghuslu?

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atuepushe na jambo hilo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share