045 - Al-Jaathiyah

 

 

 

الْجاثِيَة

Al-Jaathiyah: 045

 

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

حم﴿١﴾

1. Haa Miym

 

 

تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾

2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٣﴾

3. Hakika katika mbingu na ardhi bila shaka kuna ishara na dalili kwa Waumini.

 

 

وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٤﴾

4. Na katika kuumbwa kwenu, na Anaoyatawanya kati ya viumbe vinavyotembea ni hoja na dalili kwa watu wenye yakini.

 

 

 

وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٥﴾

5. Na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, na Anayoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika mvua, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na kugeukageuka upepo (wa Rahmah) ni ishara na dalili kwa watu wanaotia akilini.

 

 

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ اللَّـهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ﴿٦﴾

6. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki. Basi kauli gani baada ya Allaah na Aayaat Zake wataziamini?

 

 

 

وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ﴿٧﴾

7.  Ole kwa kila mzushi muongo, mtendaji mno dhambi.

 

 

 

يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّـهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٨﴾

8. Anazisikia Aayaat za Allaah akisomewa, kisha anang’ang’ana kuwa mwenye kutakabari kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu iumizayo.

 

 

 

وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ﴿٩﴾

9. Na anapojua chochote katika Aayaat Zetu huzichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

 

 

مِّن وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِي عَنْهُم مَّا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا مَا اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠﴾

10. Nyuma yao iko Jahannam, na wala hayatowafaa kitu yale waliyoyachuma na wala wale waliowafanya walinzi badala ya Allaah, na watapata adhabu kuu.

 

 

هَـٰذَا هُدًى ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ﴿١١﴾

11. Hii (Qur-aan) ni mwongozo. Na wale waliokanusha Aayaat za Rabb   wao watapata adhabu ya kufadhaika iumizayo.

 

 

 

اللَّـهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٢﴾

12. Allaah Ambaye Amekutiishieni bahari ili zipite merikebu humo kwa Amri Yake, na ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.

 

 

 

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١٣﴾

13. Na Amekutiishieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini vyote, ni ihsani itokaye Kwake. Hakika katika hayo bila shaka kuna dalili na ishara kwa watu wanaotafakari.

 

 

 

قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّـهِ لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٤﴾

14 Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji Siku za Allaah ili Awalipe watu kutokana na yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۖ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ﴿١٥﴾

15. Yeyote atendaye jema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kufanya uovu, basi ni hasara kwake, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa.

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿١٦﴾

16. Na kwa yakini Tuliwapa wana wa Israaiyl Kitabu na hikma na unabii, na Tukawaruzuku katika vizuri, na Tukawafadhilisha juu ya walimwengu.

 

 

 

وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٧﴾

17. Na Tukawapa hoja bayana ya mambo (ya Dini). Basi hawakukhitilafiana isipokuwa baada ya kuwajia ilimu kwa kufanyiana uadui na husuda baina yao. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.

 

 

 

ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٨﴾

18. Kisha Tukakuwekea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Shariy’ah ya mambo, basi ifuate, na wala usifuate hawaa za wale wasiojua.

 

 

إِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا عَنكَ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۖ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ﴿١٩﴾

19. Hakika wao hawatokufaa chochote mbele ya Allaah. Na hakika madhalimu ni marafiki wanaoshirikiana wao kwa wao. Na Allaah Ni Mlinzi wa wenye taqwa.

 

 

هَـٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٢٠﴾

20. Hii (Qur-aan) ni busara na kifumbuzi macho kwa watu, na ni mwongozo na Rahmah kwa watu wenye yakini.

 

 

 

أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٢١﴾

21. Je, wanadhania wale waliochuma maovu kwamba Tutawafanya sawa na wale walioamini na wakatenda mema, sawasawa uhai wao na kufa kwao? Uovu ulioje wa wanavyohukumu!  

 

 

 

وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٢﴾

22. Na Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili ilipwe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.

 

 

 

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٣﴾

23. Je, umemuona yule aliyejichukulia hawaa zake kuwa ndio mwabudiwa wake, na Allaah Akampotoa baada ya kufikiwa na ilimu na hoja, na Akapiga mhuri juu ya masikio yake na moyo wake, na Akaweka kifuniko juu ya macho yake? Basi nani atamuongoa baada ya Allaah? Je, basi hamkumbuki?

 

 

 

وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ﴿٢٤﴾

24. Na wakasema: Huu si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia, tunakufa na tunahuika, na hakuna cha kutuangamiza isipokuwa zama tu. Na wala hawana kwayo ujuzi wowote, ila wao wanadhania tu.

 

 

 

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾

25. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana haikuwa hoja yao isipokuwa kusema: Tuleteeni mababa zetu mkiwa nyinyi ni wakweli.

 

 

 

قُلِ اللَّـهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢٦﴾

26. Sema: Allaah Anakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah isiyo na shaka ndani yake, lakini watu wengi hawajui.

 

 

 

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ﴿٢٧﴾

27. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na Siku itakayosimama Saa, watakhasirika Siku hiyo wabatilifu.

 

 

 

وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً ۚ كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰ إِلَىٰ كِتَابِهَا الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾

28. Na utaona kila ummah umepiga magoti kwa unyenyekevu (na khofu). Kila ummah utaitwa kwenye kitabu chake (cha matendo): Leo mtalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٩﴾

29. Hiki ni kitabu Chetu, kinatamka (kushuhudia) juu yenu kwa haki. Hakika Sisi Tulikuwa Tunaamuru yaandikwe yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي رَحْمَتِهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ﴿٣٠﴾

30. Basi wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaingiza katika Rahmah Yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi.

 

 

 

وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنتُمْ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٣١﴾

31. Ama wale waliokufuru (wataambiwa): Je, kwani hazikuwa Aayaat Zangu zikisomwa kwenu, mkatakabari na mkawa watu wahalifu?

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم مَّا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ﴿٣٢﴾

32. Na inaposemwa: Hakika Ahadi ya Allaah ni haki, na Saa haina shaka ndani yake mlisema: Hatujui Saa ni nini! Hatudhanii isipokuwa ni dhana tupu, nasi sio wenye kuyakinika kikweli.

 

 

 

وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٣﴾

33. Na yatawafichukia maovu waliyoyatenda, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٤﴾

34. Na itasemwa: Leo Tunakusahauni kama mlivyosahau kukutana na Siku yenu hii, na makazi yenu ni motoni, na wala hamna yeyote mwenye kunusuru.

 

 

 

ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٣٥﴾

35. Hivyo ni kwa sababu nyinyi mlizichukulia mzaha Aayaat za Allaah, na ukakudanganyeni uhai wa dunia. Basi leo hawatotolewa humo, na wala hawataachiliwa nafasi ya kujitetea (kwa Allaah).

 

 

 

فَلِلَّـهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٦﴾

36. Basi AlhamduliLLaah  (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa mbingu na Rabb wa ardhi, Rabb wa walimwengu.

 

 

 

وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣٧﴾

37. Na Ukubwa, Uadhama, Ujalali ni Wake Pekee mbinguni na ardhini. Naye Ndiye Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

Share