046 - Al-Ahqaaf

 

 

 

  الأَحْقَاف

Al-Ahqaaf: 046

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

حم﴿١﴾

1. Haa Miym.

 

 

تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾

2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ﴿٣﴾

3. Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na kwa muda maalumu uliokadiriwa. Na waliokufuru wanayakengeuka yale wanayoonywa.

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ۖ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤﴾

4. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnawaona wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi, au wana ushirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kabla ya hiki, au alama yeyote ya ilimu mkiwa wakweli.

 

 

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾

5. Na nani aliyepotoka zaidi kuliko yule anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah? Nao wala hawatambui maombi yao!  

 

 

وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ﴿٦﴾

6. Na pale watakapokusanywa watu, (miungu ya uongo) watakuwa ni maadui wao, na watakuwa wenye kuzikanusha ‘ibaadah zao.

 

 

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾

7. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, husema wale waliokufuru kuhusu haki ilipowajia: Hii ni sihiri bayana.

 

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَلَا تَمْلِكُونَ لِي مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ ۖ كَفَىٰ بِهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۖ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٨﴾

8. Bali wanasema ameitunga. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi hamna uwezo wa kunifaa chochote mbele ya Allaah. Yeye Anajua zaidi yale mnayoyaropoka. Anatosha kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu, Naye Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٩﴾

9. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mimi sio wa mwanzo kuja na Utume miongoni mwa Rusuli, na sijui nitakavyofanyiwa mimi wala nyinyi. Sifuati isipokuwa niliyofunuliwa Wahy, nami si chochote isipokuwa ni mwonyaji bayana.

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَكَفَرْتُم بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠﴾

10. Sema: Mnaonaje ikiwa (hii Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, na mkaikanusha, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israaiyl juu ya mfano wa haya, na akaamini nanyi mkatabari? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَا إِلَيْهِ ۚ وَإِذْ لَمْ يَهْتَدُوا بِهِ فَسَيَقُولُونَ هَـٰذَا إِفْكٌ قَدِيمٌ﴿١١﴾

11. Na wale waliokufuru wakasema kuwaambia walioamini: Lau ingelikuwa ni kheri, basi wasingetusabiki. Na kwa kuwa hawakuhidika kwayo (Qur-aan), basi watasema: Huu ni uzushi wa zamani.

 

 

وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ وَهَـٰذَا كِتَابٌ مُّصَدِّقٌ لِّسَانًا عَرَبِيًّا لِّيُنذِرَ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَبُشْرَىٰ لِلْمُحْسِنِينَ﴿١٢﴾

12. Na kabla yake ni kitabu cha Muwsaa chenye kuongoza, na kuwa ni Rahmah. Na hiki Kitabu kinasadikisha kwa lugha ya Kiarabu ili kionye wale waliodhulumu, na ni bishara kwa wafanyao ihsaan.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿١٣﴾

13. Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara, basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

 

أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٤﴾

14. Hao ndio watu wa Jannah, ni wenye kudumu humo, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.

 

 

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿١٥﴾

15. Na Tumemuusia binaadamu kuwafanyia wema wazazi wake wawili. Mama yake amebeba mimba yake kwa tabu na akamzaa kwa tabu. Na kuibeba mimba na kuachishwa kwake kunyonya ni miezi thelathini. Mpaka anapofikia umri wake wa kupevuka, na akafikia miaka arubaini husema: Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Nitengenezee dhuria wangu. Hakika mimi nimetubu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ نَتَقَبَّلُ عَنْهُمْ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَنَتَجَاوَزُ عَن سَيِّئَاتِهِمْ فِي أَصْحَابِ الْجَنَّةِ ۖ وَعْدَ الصِّدْقِ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale ambao Tunawatakabalia mazuri zaidi ya yale waliyoyatenda, na Tunayaachilia mbali maovu yao, watakuwa katika watu wa Jannah. Ahadi ya kweli waliyokuwa wameahidiwa.

 

 

وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِن قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّـهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٧﴾

17. Na yule anaewaambia wazazi wake: Uff! Mnanitishia kwamba nitatolewa kufufuliwa na hali zimekwishapita karne nyingi kabla yangu! Nao wazazi wawili wanaomba uokozi kwa Allaah, na (humwambia mtoto wao): Ole wako amini! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Lakini husema: Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿١٨﴾

18. Hao ndio wale ambao imehakiki juu yao kauli (ya adhabu) kama katika nyumati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanaadamu. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika.

 

 

وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۖ وَلِيُوَفِّيَهُمْ أَعْمَالَهُمْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١٩﴾

19. Na wote watakuwa na daraja mbali mbali kutokana na yale waliyoyatenda, na ili (Allaah) Awalipe kikamilifu ‘amali zao, nao hawatodhulumiwa.

 

 

وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُم بِهَا فَالْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَفْسُقُونَ﴿٢٠﴾

20. Na siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (waambiwe): Je, mshamaliza vizuri vyenu katika uhai wenu wa dunia na mshajistarehesha navyo? Basi leo mtalipwa adhabu ya udhalilifu kwa vile mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa ufasiki mliokuwa mnaufanya.

 

 

وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿٢١﴾

21. Na mtaje (Huwd) ndugu wa kina ‘Aad alipowaonya watu wake katika nchi ya machuguu ya mchanga, na walikwishapita waonyaji kabla yake na baada yake: Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.

 

 

قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٢﴾

22. Wakasema: Je, umetujia ili utugeuzilie mbali na waabudiwa wetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.

 

 

قَالَ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَأُبَلِّغُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٣﴾

23. (Huwd) akasema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah, nami nabalighisha ambayo nimetumwa kwayo, lakini nakuoneni nyinyi ni kaumu wenye kufanya ujahili.

 

 

فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُّسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا هَـٰذَا عَارِضٌ مُّمْطِرُنَا ۚ بَلْ هُوَ مَا اسْتَعْجَلْتُم بِهِ ۖ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٤﴾

24. Basi walipoiona (adhabu waliyoihimiza) ni wingu lilotanda upeoni linaelekea mabonde yao walisema: Wingu hili lilotanda upeoni ni la kutunyeshea mvua. Bali hilo ndilo mloharakiza, ni upepo wa dhoruba ndani yake kuna adhabu iumizayo.

 

 

تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا لَا يُرَىٰ إِلَّا مَسَاكِنُهُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿٢٥﴾

25. Unadamirisha kila kitu kwa Amri ya Rabb wake. Wakapambaukiwa hayaonekani isipokuwa masikani zao tu. Hivyo ndivyo Tunavyolipa jazaa watu wahalifu.

 

وَلَقَدْ مَكَّنَّاهُمْ فِيمَا إِن مَّكَّنَّاكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَارًا وَأَفْئِدَةً فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَا أَبْصَارُهُمْ وَلَا أَفْئِدَتُهُم مِّن شَيْءٍ إِذْ كَانُوا يَجْحَدُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٢٦﴾

26. Na kwa yakini Tuliwamakinisha vizuri zaidi kuliko Tulivyokumakinisheni (nyinyi Maquraysh). Na Tukawapa masikio na macho na nyoyo za kutafakari, lakini hayakuwafaa chochote masikio yao wala macho yao wala nyoyo zao za kutafakari kwa kuwa walikuwa wakikanusha kwa ujeuri Aayaat na Ishara za Allaah, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُم مِّنَ الْقُرَىٰ وَصَرَّفْنَا الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٧﴾

27. Na kwa yakini Tuliangamiza miji iliyokuwa pembezoni mwenu, na Tukasarifu waziwazi ishara na dalili ili wapate kurejea.

 

 

فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢٨﴾

28. Basi kwa nini wasiwanusuru wale waliowafanya badala ya Allaah kuwa ni waabudiwa wa kikurubisho (Kwake)? Bali wamewapotea, na huo ndio uongo wao na yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ﴿٢٩﴾

29. Na pale Tulipowaelekeza kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم  ) kundi miongoni mwa majini ili kuisikiliza Qur-aan. Walipohudhuria majlisi, walisema: Bakieni kimya msikilize! Ilipomalizika, waligeuka kurudi kwa kaumu yao wakiwa wenye kuonya.

 

قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٠﴾

30. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣١﴾

31. Enyi kaumu yetu! Mwitikieni Mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini!  (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo.

 

 

وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٢﴾

32. Na yeyote asiyemuitikia Mlinganiaji wa Allaah, basi hawezi kushinda kukwepa katika ardhi, na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah.  Hao wamo katika upotofu bayana.

 

 

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ۚ بَلَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٣﴾

33. Je, hawaoni kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na wala Hakuchoka kwa kuziumba kwake, kwamba Yeye Ni Muweza wa Kuwafufua wafu. Naam bila shaka!  Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ﴿٣٤﴾

34. Na Siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (isemwe): Je, hii si kweli? Watasema: Bali ndio!  Tunaapa kwa Rabb wetu! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri mliokuwa mkiufanya.

 

 

فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِل لَّهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّن نَّهَارٍ ۚ بَلَاغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ﴿٣٥﴾

35. Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti miongoni mwa Rusuli, na wala usiwaharakizie. Siku watakayoona waliyoahidiwa itakuwa kama kwamba hawakubakia (duniani) isipokuwa saa moja tu katika mchana. (Huu) ni ubalighisho! Je, basi kwani huangamizwa isipokuwa watu mafasiki?

 

 

 

Share