094 - Ash-Sharh

 

 

 

  الشَّرْح

Ash-Sharh: 094

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾

1. Je, kwani Hatukukupanulia kifua chako kukubainishia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

 

وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾

2. Na Tukakuondolea mzigo wako (wa dhambi)?

 

 

الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾

3. Ambao ulielemea mgongo wako?

 

 

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

4. Na Tukakutukuzia kutajwa kwako?

 

 

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾

5. Basi hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.

 

 

إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾

6. Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.

 

 

فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾

7. Basi utakapopata faragha fanya juhudi katika ‘ibaadah.

 

 

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾

8. Na kwa ajili ya Rabb wako, ongeza utashi zaidi (wa ‘ibaadah).

 

 

 

 

Share