Skip to main content

  النَّصْر

110-An-Naswr

110-An-Naswr: Utangulizi Wa Suwrah

Alhidaaya.com

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ ﴿١﴾

1. Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.[1]

وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا ﴿٢﴾

2. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah makundi makundi.

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾

3. Basi hapo sabbih na mhimidi Rabb wako (kwa wingi zaidi) na muombe maghfirah. Hakika Yeye daima Ni Mwingi mno wa Kupokea tawbah.

 

[1] Faida Na Fadhila Za Suwrah:

Rejea Utangulizi Wa Suwrah kupata faida na fadhila ya Suwrah hii