Makaroni Ya Kamba Cooking Cream Brocoli Na Karoti

 Makaroni Ya Kamba Cooking Cream, Brocoli Na Karoti

 

 

Vipimo

 

Makaroni - 500 gramu (gms)

Kamba wa barafu (frozen) saizi ya katikati - 1000 gms

Cooking cream (krimu ya malai) - 170 gms

Maziwa ya chai ya kopo - 1/4 kikombe

Mafuta ya kukaangia - 1/4 kikombe

Vitunguu vilivyokatwa vidogodogo - 2

Karoti iliyokatwa ndogo ndogo - 1

Pilipili kubwa kata ndogo ndogo - 1

Figili mwitu (celery) kata ndogo ndogo - 2 miche

Brocoli kata vipande vipande - 1 msongo (bunch)

Nyanya iliyosagwa (au rojo ya nyanya (paste) - 1/2 kikombe

Pilipili mbuzi iliyokatwa ndogo ndogo (ukipenda) - 1

Mraba ya supu ya kuku au nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).

Chumvi - kiasi

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha supu.

 

 

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 1. Chemsha makaroni kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika karatasi.  (usiyaivishe sana hadi yakavurugika)
 2. Yakishawiva mwaaga maji kwa kuchuja.
 3. Katika sufuria kubwa au karai, tia mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu kama dakika 1 tu.
 4. Tia pilipili mboga, karoti, pilipili mbuzi.
 5. Mumunyia mraba ya Maggi (Maggi cubes)
 6. Tia nyanya iliyosagwa au rojo ya nyanya na kaanga tena kidogo tu kama dakika moja.
 7. Tia chumvi na pilipili manga.
 8. Tia kamba na ukaange kidogo tu kwani huiva mara moja.
 9. Mimina makaroni na changanya vizuri.
 10. Tia  brokoli, na figili mwitu (celery)
 11. Malizia kwa kutia cooking cream (krimu ya malai) na maziwa  na pika kwa dakika 2, ikiwa tayari kuliwa.

 

 

Share