Al-Lajnah Ad-Daaimah: Aashuraa: Swawm Siku Moja Ya ‘Aashuraa Pekee Inajuzu?

 

Swawm Siku Moja Ya ‘Aashuraa Pekee Inajuzu?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, inajuzu kufunga siku moja tu ya ‘Aashuraa?

 

JIBU:

 

Inajuzu kufunga siku ya ‘Aashuraa siku moja pekee, lakini ni bora kufunga siku kabla yake au siku baada yake kwani hivi ndio Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema:

 

“Nikiishi hadi mwakani nitafunga siku ya tisa.”  Ibn ‘Abbaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) amesema “Yaani siku ya kumi (ya Muharram)]   [Muslim, Ahmad, Ibn Maajah, Ibn Abiy Shaybah, Atw-Twahaawiy, Al-Bayhaqiy, Al-Baghaawiy]   

 

Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah 10/401 Fatwa namba 13700]

 

Share