Skip to main content

46 - Swahiyh Al-Bukhaariy Kitabu Cha Madhwaalim (Dhulma)

كِتَابُ الْمَظَالِمِ

Kitabu Cha Madhwaalim (Dhulma)

1-Mlangoباب قِصَاصِ الْمَظَالِمِMlango Wa Kisasi Cha Dhulma

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَخْبَرَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَبِي الْمُتَوَكِّلِ النَّاجِيِّ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضي الله عنه ـ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " إِذَا خَلَصَ الْمُؤْمِنُونَ مِنَ النَّارِ حُبِسُوا بِقَنْطَرَةٍ بَيْنَ الْجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَيَتَقَاصُّونَ مَظَالِمَ كَانَتْ بَيْنَهُمْ فِي الدُّنْيَا، حَتَّى إِذَا نُقُّوا وَهُذِّبُوا أُذِنَ لَهُمْ بِدُخُولِ الْجَنَّةِ، فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وآله وسلم بِيَدِهِ لأَحَدُهُمْ بِمَسْكَنِهِ فِي الْجَنَّةِ أَدَلُّ بِمَنْزِلِهِ كَانَ فِي الدُّنْيَا ". وَقَالَ يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ حَدَّثَنَا شَيْبَانُ عَنْ قَتَادَةَ حَدَّثَنَا أَبُو الْمُتَوَكِّلِ.

Ametusimulia Is-haaq bin Ibraahiym, amesema: Ametujulisha Mu'aadh bin Hishaam, amesema: Amenisimulia baba yangu, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Abul-Mutawakkil An-Naajiy, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Waumini watakapookoka kutoka motoni, watazuiliwa juu ya daraja lililo baina ya Jannah (Pepo) na moto, walipizane kisasi cha dhulma zilizokuwa baina yao duniani. Mpaka watakapotakaswa na kusafishwa, watapewa idhini ya kuingia Jannah. Basi Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake, hakika mmoja wao atayajua zaidi makazi yake katika Jannah kuliko alivyoijua nyumba yake aliyokuwa nayo duniani.”

Na Yuwnus bin Muhammad amesema: Ametusimulia Shaybaan, kutoka kwa Qataadah: Ametusimulia Abul-Mutawakkil.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
128
Hadiyth
2440

2-Mlangoبَابُ قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى: {أَلاَ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ}Mlango Wa Kauli Ya Allaah (تعالى): {Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu} [Huud (11:18)]

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، قَالَ أَخْبَرَنِي قَتَادَةُ، عَنْ صَفْوَانَ بْنِ مُحْرِزٍ الْمَازِنِيِّ، قَالَ بَيْنَمَا أَنَا أَمْشِي، مَعَ ابْنِ عُمَرَ ـ رضي الله عنهما ـ آخِذٌ بِيَدِهِ إِذْ عَرَضَ رَجُلٌ، فَقَالَ كَيْفَ سَمِعْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم فِي النَّجْوَى فَقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ " إِنَّ اللَّهَ يُدْنِي الْمُؤْمِنَ فَيَضَعُ عَلَيْهِ كَنَفَهُ، وَيَسْتُرُهُ فَيَقُولُ أَتَعْرِفُ ذَنْبَ كَذَا أَتَعْرِفُ ذَنْبَ كَذَا فَيَقُولُ نَعَمْ أَىْ رَبِّ. حَتَّى إِذَا قَرَّرَهُ بِذُنُوبِهِ وَرَأَى فِي نَفْسِهِ أَنَّهُ هَلَكَ قَالَ سَتَرْتُهَا عَلَيْكَ فِي الدُّنْيَا، وَأَنَا أَغْفِرُهَا لَكَ الْيَوْمَ. فَيُعْطَى كِتَابَ حَسَنَاتِهِ، وَأَمَّا الْكَافِرُ وَالْمُنَافِقُونَ فَيَقُولُ الأَشْهَادُ هَؤُلاَءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى رَبِّهِمْ، أَلاَ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ".

Ametusimulia Muwsaa bin Ismaa'iyl, amesema: Ametusimulia Hammaam, amesema: Amenijulisha Qataadah, kutoka kwa Swafwaan bin Muhriz Al-Maaziniy, amesema: Nilipokuwa nikitembea pamoja na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), nikiwa nimeushika mkono wake, ghafla akajitokeza mtu mmoja, akasema: Ulimsikiaje Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (akisema) kuhusu An-Najwaa (mazungumzo ya siri baina ya Allaah na Mja Wake Siku ya Qiyaamah)? Akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Hakika Allaah Humkurubisha Muumini, Akamwekea sitara Yake (kanafa Yake), na Akamsitiri, kisha Anasema: Je, unaijua dhambi fulani? Je, unaijua dhambi fulani? Naye anasema: Naam, yaa Rabb wangu. Mpaka Atakapomkiririsha dhambi zake, naye akaona nafsini mwake kwamba ameangamia, (Allaah) Husema: Nilikusitiria dhambi hizo duniani, na Mimi Nakughufuria leo. Kisha anapewa kitabu cha mema yake. Ama kafiri na wanafiki, mashahidi watasema:

هَؤُلاَءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى رَبِّهِمْ، أَلاَ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ

Hawa ndio wale waliomzulia uongo Rabb wao! Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu [Huud (11:18)]

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
128
Hadiyth
2441

3-Mlangoباب لاَ يَظْلِمُ الْمُسْلِمُ الْمُسْلِمَ وَلاَ يُسْلِمُهُMlango Wa Muislamu Hamdhulumu Muislamu (Mwenzake) Wala Hamtelekezi

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، أَنَّ سَالِمًا، أَخْبَرَهُ أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ ـ رضي الله عنهما ـ أَخْبَرَهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللَّهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ".

Ametusimulia Yahyaa bin Bukayr, amesema: Ametusimulia Al-Layth, kutoka kwa 'Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, kwamba Saalim alimjulisha kwamba 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما) alimjulisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muislamu ni ndugu wa Muislamu; hamdhulumu wala hamtelekezi (kwa anayemdhuru). Na mwenye kuwa katika (kukidhi) haja ya nduguye, Allaah Atakuwa katika (kukidhi) haja yake. Na mwenye kumwondolea Muislamu dhiki, Allaah Atamwondolea dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
128
Hadiyth
2442

4-Mlangoباب أَعِنْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًاMlango Wa Msaidie Nduguyo Akiwa Dhalimu Au Akiwa Amedhulumiwa

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرِ بْنِ أَنَسٍ، وَحُمَيْدٌ الطَّوِيلُ، سَمِعَا أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ ـ رضي الله عنه ـ يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم " انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا ".

Ametusimulia 'Uthmaan bin Abiy Shaybah, amesema: Ametusimulia Hushaym, amesema: Ametujulisha 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Bakr bin Anas, na Humayd At-Twawiyl, (wote wawili) walimsikia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnusuru nduguyo akiwa dhalimu au akiwa amedhulumiwa.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
128
Hadiyth
2443

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ حُمَيْدٍ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم " انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا ". قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ هَذَا نَنْصُرُهُ مَظْلُومًا، فَكَيْفَ نَنْصُرُهُ ظَالِمًا قَالَ " تَأْخُذُ فَوْقَ يَدَيْهِ ".

Ametusimulia Musaddad, amesema: Ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnusuru nduguyo akiwa dhalimu au akiwa amedhulumiwa.” Wakasema: Yaa Rasula-Allaah! Huyu tunamnusuru akiwa amedhulumiwa; basi vipi tutamnusuru akiwa dhalimu? Akasema: “Unaishika mikono yake (unamzuia asidhulumu).”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
128
Hadiyth
2444

5-Mlangoباب نَصْرِ الْمَظْلُومِMlango Wa Kumnusuru Aliyedhulumiwa

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الأَشْعَثِ بْنِ سُلَيْمٍ، قَالَ سَمِعْتُ مُعَاوِيَةَ بْنَ سُوَيْدٍ، سَمِعْتُ الْبَرَاءَ بْنَ عَازِبٍ ـ رضي الله عنهما ـ قَالَ أَمَرَنَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم بِسَبْعٍ، وَنَهَانَا عَنْ سَبْعٍ. فَذَكَرَ عِيَادَةَ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعَ الْجَنَائِزِ، وَتَشْمِيتَ الْعَاطِسِ، وَرَدَّ السَّلاَمِ، وَنَصْرَ الْمَظْلُومِ، وَإِجَابَةَ الدَّاعِي، وَإِبْرَارَ الْمُقْسِمِ.

Ametusimulia Sa'iyd bin Ar-Rabiy', amesema: Ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Ash'ath bin Sulaym, amesema: Nilimsikia Mu'aawiyah bin Suwayd (akisema): Nilimsikia Al-Baraa bin 'Aazib (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha mambo saba, na akatukataza mambo saba. Akataja: Kumtembelea mgonjwa, kufuata majeneza, kumwombea mwenye kupiga chafya (tashmiyt), kuitikia Salaam, kumnusuru aliyedhulumiwa, kumwitikia mwenye kualika, na kutimiza kiapo cha mwenye kuapa.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
129
Hadiyth
2445

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلاَءِ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ بُرَيْدٍ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى ـ رضي الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " الْمُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا ". وَشَبَّكَ بَيْنَ أَصَابِعِهِ.

Ametusimulia Muhammad bin Al-'Alaa, amesema: Ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Burayd, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Muumini kwa Muumini ni kama jengo; sehemu yake moja huikaza nyingine.” Na akafumanisha vidole vyake (vya mikono miwili).

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
129
Hadiyth
2446

6-Mlangoبَابُ الاِنْتِصَارِ مِنَ الظَّالِمِMlango Wa Kujitetea Dhidi Ya Dhalimu

Kwa sababu ya Kauli Yake (جلّ ذكره):

لاَ يُحِبُّ اللَّهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلاَّ مَنْ ظُلِمَ وَكَانَ اللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا

Allaah Hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote [An-Nisaa (4:148)]

Na:

وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنْتَصِرُونَ

Na wale wanapokabiliwa na baghi (ukandamizaji na dhulma), wao wanajitetea [Ash-Shuuraa (42:39)]

Ibraahiym amesema: Walikuwa wakichukia kudhalilishwa, na walipokuwa na uwezo (wa kulipiza), walisamehe.

7-Mlangoبَابُ عَفْوِ الْمَظْلُومِMlango Wa Kusamehe Kwa Aliyedhulumiwa

Kwa sababu ya Kauli Yake (تعالى):

إِنْ تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَنْ سُوءٍ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا

Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu, basi hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Muweza wa yote [An-Nisaa (4:149)]

Na:

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِثْلُهَا فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ إِنَّهُ لاَ يُحِبُّ الظَّالِمِينَ وَلَمَنِ انْتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَئِكَ مَا عَلَيْهِمْ مِنْ سَبِيلٍ إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَلَمَنْ صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الأُمُورِ

Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini atakayesamehe na akajenga mahusiano mema na aliyemkosea, basi ujira wake uko kwa Allaah. Hakika Yeye Hapendi madhalimu. Na bila shaka anayelipiza kisasi baada ya kudhulumiwa, basi hao hawana sababu ya kulaumiwa. Hakika sababu (ya kulaumiwa) ni juu ya wale wanaodhulumu watu na wanafanya baghi (ukandamizaji) katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iumizayo. Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa [Ash-Shuuraa (42:40-43)]

Na:

وَتَرَى الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَى مَرَدٍّ مِنْ سَبِيلٍ

Na utawaona madhalimu watakapoiona adhabu wakisema: Je, ipo njia yoyote ya kurudi (duniani)? [Ash-Shuuraa (42:44)]

8-Mlangoباب الظُّلْمُ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِMlango Wa Dhulma Ni Viza Siku Ya Qiyaamah

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ الْمَاجِشُونُ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دِينَارٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ ـ رضي الله عنهما ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " الظُّلْمُ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ".

Ametusimulia Ahmad bin Yuwnus, amesema: Ametusimulia 'Abdul-'Aziyz Al-Maajishuwn, amesema: Ametujulisha 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Dhulma ni viza Siku ya Qiyaamah.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
129
Hadiyth
2447

9-Mlangoباب الاِتِّقَاءِ وَالْحَذَرِ مِنْ دَعْوَةِ الْمَظْلُومِMlango Wa Kujikinga Na Kutahadhari Na Du'aa Ya Aliyedhulumiwa

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّاءُ بْنُ إِسْحَاقَ الْمَكِّيُّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ صَيْفِيٍّ، عَنْ أَبِي مَعْبَدٍ، مَوْلَى ابْنِ عَبَّاسٍ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضي الله عنهما ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ، فَقَالَ " اتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ، فَإِنَّهَا لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ ".

Ametusimulia Yahyaa bin Muwsaa, amesema: Ametusimulia Wakiy', amesema: Ametusimulia Zakariyyaa bin Is-haaq Al-Makkiy, kutoka kwa Yahyaa bin 'Abdi-Allaah bin Swayfiyy, kutoka kwa Abuw Ma'bad mwachwa huru wa Ibn 'Abbaas, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtuma Mu'aadh (رضي الله عنه) Yemen, akasema: “Iogope Du'aa ya aliyedhulumiwa, kwani hakuna kizuizi baina yake na Allaah.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
129
Hadiyth
2448

10-Mlangoباب مَنْ كَانَتْ لَهُ مَظْلَمَةٌ عِنْدَ الرَّجُلِ فَحَلَّلَهَا لَهُ، هَلْ يُبَيِّنُ مَظْلَمَتَهُMlango Wa Aliyekuwa Na Dhulma (Aliyofanyiwa) Kwa Mtu, Kisha Akamsamehe, Je, Aibainishe Dhulma Hiyo?

حَدَّثَنَا آدَمُ بْنُ أَبِي إِيَاسٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ الْمَقْبُرِيُّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم " مَنْ كَانَتْ لَهُ مَظْلَمَةٌ لأَحَدٍ مِنْ عِرْضِهِ أَوْ شَىْءٍ فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ الْيَوْمَ، قَبْلَ أَنْ لاَ يَكُونَ دِينَارٌ وَلاَ دِرْهَمٌ، إِنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلَمَتِهِ، وَإِنْ لَمْ تَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ فَحُمِلَ عَلَيْهِ ". قَالَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ قَالَ إِسْمَاعِيلُ بْنُ أَبِي أُوَيْسٍ إِنَّمَا سُمِّيَ الْمَقْبُرِيَّ لأَنَّهُ كَانَ نَزَلَ نَاحِيَةَ الْمَقَابِرِ. قَالَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ وَسَعِيدٌ الْمَقْبُرِيُّ هُوَ مَوْلَى بَنِي لَيْثٍ، وَهُوَ سَعِيدُ بْنُ أَبِي سَعِيدٍ، وَاسْمُ أَبِي سَعِيدٍ كَيْسَانُ.

Ametusimulia Aadam bin Abiy Iyaas, amesema: Ametusimulia Ibn Abiy Dhi'b, amesema: Ametusimulia Sa'iyd Al-Maqburiy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuwa na dhulma aliyomfanyia mtu, katika heshima yake au katika kitu (kingine), basi amwombe amsamehe leo, kabla haijafika (siku) ambayo hakutakuwa na diynaar (sarafu ya dhahabu) wala dirhamu (sarafu ya fedha). Ikiwa ana amali njema, itachukuliwa kutoka kwake kwa kadiri ya dhulma yake; na ikiwa hana mema, yatachukuliwa (baadhi ya) maovu ya mwenzake (aliyedhulumiwa), na atabebeshwa.”

Amesema Abuw 'Abdi-Allaah: Ismaa'iyl bin Abiy Uways amesema: Aliitwa Al-Maqburiy kwa sababu alikuwa ameshukia (kuishi) upande wa makaburi (al-maqaabir).

Amesema Abuw 'Abdi-Allaah: Na Sa'iyd Al-Maqburiy ni mwachwa huru wa Banu Layth, naye ni Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd, na jina la Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه) ni Kaysaan.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
129
Hadiyth
2449

11-Mlangoباب إِذَا حَلَّلَهُ مِنْ ظُلْمِهِ فَلاَ رُجُوعَ فِيهِMlango Wa Akimsamehe Dhulma Yake, Basi Hakuna Kurejea Katika Hilo

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، أَخْبَرَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضي الله عنها – {وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِنْ بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا} قَالَتِ الرَّجُلُ تَكُونُ عِنْدَهُ الْمَرْأَةُ، لَيْسَ بِمُسْتَكْثِرٍ مِنْهَا، يُرِيدُ أَنْ يُفَارِقَهَا، فَتَقُولُ أَجْعَلُكَ مِنْ شَأْنِي فِي حِلٍّ. فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِي ذَلِكَ.

Ametusimulia Muhammad, amesema: Ametujulisha 'Abdu-Allaah, amesema: Ametujulisha Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) (kuhusu Kauli Yake Allaah):

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِنْ بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa [An-Nisaa (4:128)]

Amesema: Ni mwanamume ambaye yuko na mke, (lakini) hampendi sana, anataka kumwacha; naye (mke) anasema: Nimekuweka huru katika haki zangu (nimekusamehe haki zangu). Basi ikateremka Aayah hii kuhusu hilo.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2450

12-Mlangoباب إِذَا أَذِنَ لَهُ أَوْ أَحَلَّهُ وَلَمْ يُبَيِّنْ كَمْ هُوَMlango Wa Akimpa Idhini Au Akimsamehe Bila Kubainisha Ni Kiasi Gani

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي حَازِمِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ ـ رضي الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم أُتِيَ بِشَرَابٍ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَعَنْ يَمِينِهِ غُلاَمٌ وَعَنْ يَسَارِهِ الأَشْيَاخُ، فَقَالَ لِلْغُلاَمِ " أَتَأْذَنُ لِي أَنْ أُعْطِيَ هَؤُلاَءِ ". فَقَالَ الْغُلاَمُ لاَ وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ لاَ أُوثِرُ بِنَصِيبِي مِنْكَ أَحَدًا. قَالَ فَتَلَّهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم فِي يَدِهِ.

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yuwsuf, amesema: Ametujulisha Maalik, kutoka kwa Abuw Haazim bin Diynaar, kutoka kwa Sahl bin Sa'd As-Saa'idiy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa kinywaji, akanywa, na kuliani kwake alikuwa kijana, na kushotoni kwake wazee. Akamwambia yule kijana: “Je, unanipa idhini niwape hawa?” Yule kijana akasema: Hapana, Wa-Allaahi, Yaa Rasula-Allaah! Sitampa yeyote kipaumbele juu ya sehemu yangu itokayo kwako. (Sahl) amesema: Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akakiweka mkononi mwake [yule kijana].

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2451

13-Mlangoباب إِثْمِ مَنْ ظَلَمَ شَيْئًا مِنَ الأَرْضِMlango Wa Dhambi Ya Mwenye Kudhulumu Kitu Katika Ardhi

حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ حَدَّثَنِي طَلْحَةُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ عَمْرِو بْنِ سَهْلٍ، أَخْبَرَهُ أَنَّ سَعِيدَ بْنَ زَيْدٍ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ " مَنْ ظَلَمَ مِنَ الأَرْضِ شَيْئًا طُوِّقَهُ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ ".

Ametusimulia Abul-Yamaan, amesema: Ametujulisha Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenisimulia Twalhah bin 'Abdi-Allaah, kwamba 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr bin Sahl alimjulisha kwamba Sa'iyd bin Zayd (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mwenye kudhulumu kitu katika ardhi, atavalishwa shingoni (kipande hicho) kutoka ardhi saba.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2452

حَدَّثَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، حَدَّثَنَا حُسَيْنٌ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنَّ أَبَا سَلَمَةَ، حَدَّثَهُ أَنَّهُ، كَانَتْ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أُنَاسٍ خُصُومَةٌ، فَذَكَرَ لِعَائِشَةَ ـ رضي الله عنها ـ فَقَالَتْ يَا أَبَا سَلَمَةَ اجْتَنِبِ الأَرْضَ، فَإِنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " مَنْ ظَلَمَ قِيدَ شِبْرٍ مِنَ الأَرْضِ طُوِّقَهُ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ ".

Ametusimulia Abuw Ma'mar, amesema: Ametusimulia 'Abdul-Waarith, amesema: Ametusimulia Husayn, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, amesema: Amenisimulia Muhammad bin Ibraahiym, kwamba Abuw Salamah alimsimulia kwamba kulikuwa na ugomvi baina yake na watu fulani, akamtajia 'Aaishah (رضي الله عنها) (jambo hilo). Akasema: Yaa Abaa Salamah! Jiepushe na ardhi (ya watu), kwani Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kudhulumu kiasi cha shibiri moja ya ardhi, atavalishwa shingoni (kipande hicho) kutoka ardhi saba.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2453

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ عُقْبَةَ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم " مَنْ أَخَذَ مِنَ الأَرْضِ شَيْئًا بِغَيْرِ حَقِّهِ خُسِفَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِلَى سَبْعِ أَرَضِينَ ". قَالَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ هَذَا الْحَدِيثُ لَيْسَ بِخُرَاسَانَ فِي كِتَابِ ابْنِ الْمُبَارِكِ، أَمْلاَهُ عَلَيْهِمْ بِالْبَصْرَةِ.

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, amesema: Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, amesema: Ametusimulia Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuchukua kitu katika ardhi bila ya haki yake, atadidimizwa nacho Siku ya Qiyaamah mpaka (chini ya) ardhi saba.”

Amesema Abuw 'Abdi-Allaah: Hadiyth hii haimo katika kitabu cha Ibn Al-Mubaarak (kilichoko) Khuraasaan; aliwasomea (wakaiandika) huko Al-Baswrah.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2454

14-Mlangoباب إِذَا أَذِنَ إِنْسَانٌ لآخَرَ شَيْئًا جَازَMlango Wa Mtu Akimpa Mwingine Idhini Ya Kitu, Inajuzu

حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ جَبَلَةَ، كُنَّا بِالْمَدِينَةِ فِي بَعْضِ أَهْلِ الْعِرَاقِ، فَأَصَابَنَا سَنَةٌ، فَكَانَ ابْنُ الزُّبَيْرِ يَرْزُقُنَا التَّمْرَ، فَكَانَ ابْنُ عُمَرَ ـ رضي الله عنهما ـ يَمُرُّ بِنَا فَيَقُولُ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم نَهَى عَنِ الإِقْرَانِ، إِلاَّ أَنْ يَسْتَأْذِنَ الرَّجُلُ مِنْكُمْ أَخَاهُ.

Ametusimulia Hafsw bin 'Umar, amesema: Ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Jabalah: Tulikuwa Madiynah pamoja na baadhi ya watu wa 'Iraaq, tukapatwa na mwaka (wa ukame na njaa). Na Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما) alikuwa akitupa tende kama riziki (yetu). Na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akitupita, akisema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza al-iqraan (kula tende mbili mbili kwa pamoja), isipokuwa mtu miongoni mwenu amwombe idhini nduguye.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
130
Hadiyth
2455

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ، أَنَّ رَجُلاً، مِنَ الأَنْصَارِ يُقَالُ لَهُ أَبُو شُعَيْبٍ كَانَ لَهُ غُلاَمٌ لَحَّامٌ فَقَالَ لَهُ أَبُو شُعَيْبٍ اصْنَعْ لِي طَعَامَ خَمْسَةٍ لَعَلِّي أَدْعُو النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم خَامِسَ خَمْسَةٍ. وَأَبْصَرَ فِي وَجْهِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم الْجُوعَ ـ فَدَعَاهُ، فَتَبِعَهُمْ رَجُلٌ لَمْ يُدْعَ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم " إِنَّ هَذَا قَدِ اتَّبَعَنَا أَتَأْذَنُ لَهُ ". قَالَ نَعَمْ.

Ametusimulia Abun-Nu'maan, amesema: Ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Abuw Mas'uwd (رضي الله عنه), kwamba mtu mmoja miongoni mwa Answaar aitwaye Abuw Shu'ayb alikuwa na kijana wake aliyekuwa mchinjaji. Abuw Shu'ayb akamwambia: Nitengenezee chakula kinachotosha watu watano, huenda nikamwalika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa wa tano kati ya watano. Na alikuwa ameiona njaa katika uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akamwalika, na mtu mmoja ambaye hakualikwa akawafuata. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika huyu ametufuata; je, unampa idhini?” Akasema: Naam.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2456

15-Mlangoباب قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى {وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ}Mlango Wa Kauli Ya Allaah (تعالى): {na hali yeye ni mpinzani muovu zaidi} [Al-Baqarah (2:204)]

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنِ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضي الله عنها ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللَّهِ الأَلَدُّ الْخَصِمُ ".

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Hakika mtu anayechukiwa zaidi na Allaah Ni mpinzani muovu zaidi, mgomvi sugu.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2457

16-Mlangoباب إِثْمِ مَنْ خَاصَمَ فِي بَاطِلٍ وَهْوَ يَعْلَمُهُMlango Wa Dhambi Ya Mwenye Kugombana Katika Batili Naye Anajua

حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ صَالِحٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، أَنَّ زَيْنَبَ بِنْتَ أُمِّ سَلَمَةَ، أَخْبَرَتْهُ أَنَّ أُمَّهَا أُمَّ سَلَمَةَ ـ رضي الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم أَخْبَرَتْهَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم أَنَّهُ سَمِعَ خُصُومَةً بِبَابِ حُجْرَتِهِ، فَخَرَجَ إِلَيْهِمْ، فَقَالَ " إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ وَإِنَّهُ يَأْتِينِي الْخَصْمُ، فَلَعَلَّ بَعْضَكُمْ أَنْ يَكُونَ أَبْلَغَ مِنْ بَعْضٍ، فَأَحْسِبُ أَنَّهُ صَدَقَ، فَأَقْضِيَ لَهُ بِذَلِكَ، فَمَنْ قَضَيْتُ لَهُ بِحَقِّ مُسْلِمٍ فَإِنَّمَا هِيَ قِطْعَةٌ مِنَ النَّارِ، فَلْيَأْخُذْهَا أَوْ فَلْيَتْرُكْهَا ".

Ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin 'Abdi-Allaah, amesema: Amenisimulia Ibraahiym bin Sa'd, kutoka kwa Swaalih, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: Amenijulisha 'Urwah bin Az-Zubayr kwamba Zaynab binti Ummi Salamah alimjulisha kwamba mama yake Ummu Salamah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), alimjulisha kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yeye alisikia ugomvi mlangoni pa chumba chake, akawatokea, akasema: “Hakika mimi ni mwanaadam tu, na hakika hunijia mwenye kugombana, na huenda baadhi yenu akawa fasaha zaidi (katika kujieleza) kuliko mwingine, nikadhani kwamba amesema kweli, nikamhukumia kwa hilo. Basi yeyote nitakayemhukumia (kupewa) haki ya Muislamu (mwingine), basi hakika hicho ni kipande cha moto; akichukue au akiache.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2458

17-Mlangoباب إِذَا خَاصَمَ فَجَرَMlango Wa Akizozana Hufanya Uovu

حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ خَالِدٍ، أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُرَّةَ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو ـ رضي الله عنهما ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا، أَوْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْ أَرْبَعَةٍ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ، حَتَّى يَدَعَهَا إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ ".

Ametusimulia Bishr bin Khaalid, amesema: Ametujulisha Muhammad, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin Murrah, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Mambo manne, mwenye kuwa nayo huwa mnafiki; au atakayekuwa na sifa moja katika hayo manne, huwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiahidi huvunja ahadi, na akiweka agano hulivunja kwa hila, na akizozana hufanya uovu.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2459

18-Mlangoباب قِصَاصِ الْمَظْلُومِ إِذَا وَجَدَ مَالَ ظَالِمِهِMlango Wa Aliyedhulumiwa Kulipiza Kisasi Anapoipata Mali Ya Aliyemdhulumu

حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، حَدَّثَنِي عُرْوَةُ، أَنَّ عَائِشَةَ ـ رضي الله عنها ـ قَالَتْ جَاءَتْ هِنْدُ بِنْتُ عُتْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ، فَقَالَتْ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ مِسِّيكٌ، فَهَلْ عَلَىَّ حَرَجٌ أَنْ أُطْعِمَ مِنَ الَّذِي لَهُ عِيَالَنَا فَقَالَ " لاَ حَرَجَ عَلَيْكِ أَنْ تُطْعِمِيهِمْ بِالْمَعْرُوفِ ".

Ametusimulia Abul-Yamaan, amesema: Ametujulisha Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy: Amenisimulia 'Urwah kwamba 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Alikuja Hind binti 'Utbah bin Rabiy'ah, akasema: Yaa Rasula-Allaah! Hakika Abuw Sufyaan ni mtu bakhili sana; je, ni dhambi juu yangu nikiwalisha wategemezi wetu kutoka katika (mali) yake? Akasema: “Si dhambi juu yako kuwalisha kwa kadiri ya kukubalika kisharia.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2460

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، قَالَ حَدَّثَنِي يَزِيدُ، عَنْ أَبِي الْخَيْرِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قُلْنَا لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم إِنَّكَ تَبْعَثُنَا فَنَنْزِلُ بِقَوْمٍ لاَ يَقْرُونَا فَمَا تَرَى فِيهِ فَقَالَ لَنَا " إِنْ نَزَلْتُمْ بِقَوْمٍ، فَأُمِرَ لَكُمْ بِمَا يَنْبَغِي لِلضَّيْفِ فَاقْبَلُوا، فَإِنْ لَمْ يَفْعَلُوا فَخُذُوا مِنْهُمْ حَقَّ الضَّيْفِ ".

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yuwsuf, amesema: Ametusimulia Al-Layth, amesema: Amenisimulia Yaziyd, kutoka kwa Abul-Khayr, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Tulimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika wewe unatutuma, nasi tunashukia kwa watu ambao hawatukirimu (kama wageni); basi unaonaje katika hilo? Akatuambia: “Mkishukia kwa watu, wakaamrisha mpewe kinachomstahiki mgeni, basi kubalini. Na wasipofanya hivyo, basi chukueni kutoka kwao haki ya mgeni.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
131
Hadiyth
2461

19-Mlangoباب مَا جَاءَ فِي السَّقَائِفِMlango Wa Yaliyopokewa Kuhusu As-Saqaaif (Vibanda Vya Kivuli)

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سُلَيْمَانَ، قَالَ حَدَّثَنِي ابْنُ وَهْبٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مَالِكٌ،. وَأَخْبَرَنِي يُونُسُ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، أَخْبَرَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ، أَخْبَرَهُ عَنْ عُمَرَ ـ رضي الله عنهم ـ قَالَ حِينَ تَوَفَّى اللَّهُ نَبِيَّهُ صلى الله عليه وآله وسلم إِنَّ الأَنْصَارَ اجْتَمَعُوا فِي سَقِيفَةِ بَنِي سَاعِدَةَ، فَقُلْتُ لأَبِي بَكْرٍ انْطَلِقْ بِنَا. فَجِئْنَاهُمْ فِي سَقِيفَةِ بَنِي سَاعِدَةَ.

Ametusimulia Yahyaa bin Sulaymaan, amesema: Amenisimulia Ibn Wahb, amesema: Amenisimulia Maalik. Na amenijulisha Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab: Amenijulisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah kwamba Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alimjulisha kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنهم), amesema: Allaah Alipomfisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), hakika Answaar walikusanyika katika Saqiyfah (kibanda cha kivuli) ya Banu Saa'idah. Nikamwambia Abuw Bakr (رضي الله عنه): Twende nasi. Tukawajia katika Saqiyfah ya Banu Saa'idah.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
132
Hadiyth
2462

20-Mlangoباب لاَ يَمْنَعُ جَارٌ جَارَهُ أَنْ يَغْرِزَ خَشَبَهُ فِي جِدَارِهِMlango Wa Jirani Asimzuie Jirani Yake Kuchomeka Boriti Yake Katika Ukuta Wake

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، عَنْ مَالِكٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " لاَ يَمْنَعُ جَارٌ جَارَهُ أَنْ يَغْرِزَ خَشَبَهُ فِي جِدَارِهِ ". ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ مَا لِي أَرَاكُمْ عَنْهَا مُعْرِضِينَ وَاللَّهِ لأَرْمِيَنَّ بِهَا بَيْنَ أَكْتَافِكُمْ.

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Maslamah, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jirani asimzuie jirani yake kuchomeka boriti yake (ya mbao) katika ukuta wake.” Kisha Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) husema: Nina nini nawaona mkiipuuza (Sunnah hii)? Wa-Allaahi, nitaitupa baina ya mabega yenu (nitawalazimisha nayo).

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
132
Hadiyth
2463

21-Mlangoباب صَبِّ الْخَمْرِ فِي الطَّرِيقِMlango Wa Kumwaga Khamr Njiani

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحِيمِ أَبُو يَحْيَى، أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا ثَابِتٌ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضي الله عنه ـ كُنْتُ سَاقِيَ الْقَوْمِ فِي مَنْزِلِ أَبِي طَلْحَةَ، وَكَانَ خَمْرُهُمْ يَوْمَئِذٍ الْفَضِيخَ، فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم مُنَادِيًا يُنَادِي " أَلاَ إِنَّ الْخَمْرَ قَدْ حُرِّمَتْ ". قَالَ فَقَالَ لِي أَبُو طَلْحَةَ اخْرُجْ فَأَهْرِقْهَا، فَخَرَجْتُ فَهَرَقْتُهَا، فَجَرَتْ فِي سِكَكِ الْمَدِينَةِ فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ قَدْ قُتِلَ قَوْمٌ وَهْىَ فِي بُطُونِهِمْ. فَأَنْزَلَ اللَّهُ {لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا} الآيَةَ.

Ametusimulia Muhammad bin 'Abdir-Rahiym Abuw Yahyaa, amesema: Ametujulisha 'Affaan, amesema: Ametusimulia Hammaad bin Zayd, amesema: Ametusimulia Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه): Nilikuwa mnyweshaji wa watu katika nyumba ya Abuw Twalhah (رضي الله عنه), na khamr (pombe) yao siku hizo ilikuwa al-fadhwiykh (kinywaji cha tende changa zilizopondwa). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha mtangazaji atangaze: “Tanabahi! Hakika khamr imeharamishwa.” (Anas (رضي الله عنه)) amesema: Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akaniambia: Toka nje uimwage. Nikatoka nikaimwaga, ikatiririka katika njia za Madiynah. Baadhi ya watu wakasema: Wameuawa watu (vitani) nayo (khamr) iko matumboni mwao. Basi Allaah Akateremsha:

لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا

Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharamishwa) [Al-Maaidah (5:93)]

…mpaka mwisho wa Aayah.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
132
Hadiyth
2464

22-Mlangoباب أَفْنِيَةِ الدُّورِ وَالْجُلُوسِ فِيهَا وَالْجُلُوسِ عَلَى الصُّعُدَاتِMlango Wa Viwanja Vya Nyumba Na Kukaa Humo, Na Kukaa Juu Ya Njia (As-Su'udaat)

حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ فَضَالَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو عُمَرَ، حَفْصُ بْنُ مَيْسَرَةَ عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضي الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " إِيَّاكُمْ وَالْجُلُوسَ عَلَى الطُّرُقَاتِ ". فَقَالُوا مَا لَنَا بُدٌّ، إِنَّمَا هِيَ مَجَالِسُنَا نَتَحَدَّثُ فِيهَا. قَالَ " فَإِذَا أَبَيْتُمْ إِلاَّ الْمَجَالِسَ فَأَعْطُوا الطَّرِيقَ حَقَّهَا " قَالُوا وَمَا حَقُّ الطَّرِيقِ قَالَ " غَضُّ الْبَصَرِ، وَكَفُّ الأَذَى، وَرَدُّ السَّلاَمِ، وَأَمْرٌ بِالْمَعْرُوفِ، وَنَهْىٌ عَنِ الْمُنْكَرِ ".

Ametusimulia Mu'aadh bin Fadhwaalah, amesema: Ametusimulia Abuw 'Umar Hafsw bin Maysarah, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Tahadharini na kukaa njiani.” Wakasema: Hatuna budi (nayo); hakika hizo ni mabaraza yetu tunazungumza humo. Akasema: “Basi mkikataa isipokuwa kukaa mabarazani, ipeni njia haki yake.” Wakasema: Na ni ipi haki ya njia? Akasema: “Kuinamisha macho, kuzuia udhia, kuitikia Salaam, kuamrisha mema, na kukataza maovu.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
132
Hadiyth
2465

23-Mlangoباب الآبَارِ عَلَى الطُّرُقِ إِذَا لَمْ يُتَأَذَّ بِهَاMlango Wa Visima Vilivyo Njiani Visipoleta Udhia

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، عَنْ مَالِكٍ، عَنْ سُمَىٍّ، مَوْلَى أَبِي بَكْرٍ عَنْ أَبِي صَالِحٍ السَّمَّانِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " بَيْنَا رَجُلٌ بِطَرِيقٍ، اشْتَدَّ عَلَيْهِ الْعَطَشُ فَوَجَدَ بِئْرًا فَنَزَلَ فِيهَا فَشَرِبَ، ثُمَّ خَرَجَ، فَإِذَا كَلْبٌ يَلْهَثُ يَأْكُلُ الثَّرَى مِنَ الْعَطَشِ، فَقَالَ الرَّجُلُ لَقَدْ بَلَغَ هَذَا الْكَلْبَ مِنَ الْعَطَشِ مِثْلُ الَّذِي كَانَ بَلَغَ مِنِّي، فَنَزَلَ الْبِئْرَ، فَمَلأَ خُفَّهُ مَاءً، فَسَقَى الْكَلْبَ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ ". قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ وَإِنَّ لَنَا فِي الْبَهَائِمِ لأَجْرًا فَقَالَ " فِي كُلِّ ذَاتِ كَبِدٍ رَطْبَةٍ أَجْرٌ ".

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Maslamah, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Sumayy mwachwa huru wa Abuw Bakr, kutoka kwa Abuw Swaalih As-Sammaan, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtu mmoja alipokuwa njiani, kiu ilimzidia, akakuta kisima, akateremka ndani yake akanywa, kisha akatoka. Mara (akamwona) mbwa anahema, akila udongo wenye unyevu kutokana na kiu. Yule mtu akasema: Hakika mbwa huyu amefikiwa na kiu kama ile iliyonifikia mimi. Akateremka kisimani, akajaza khuff yake (soksi ya ngozi) maji, akamnywesha mbwa. Basi Allaah Akamshukuru, Akamghufuria.” Wakasema: Yaa Rasula-Allaah! Je, hakika sisi tuna ujira hata katika wanyama? Akasema: “Katika kila (kiumbe) mwenye ini bichi (lililo hai) kuna ujira.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
132
Hadiyth
2466

24-Mlangoبَابُ إِمَاطَةِ الأَذَىMlango Wa Kuondoa Udhia (Njiani)

Na Hammaam amesema, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “(Mtu) kuondoa udhia njiani ni swadaka.”

25-Mlangoباب الْغُرْفَةِ وَالْعُلِّيَّةِ الْمُشْرِفَةِ وَغَيْرِ الْمُشْرِفَةِ فِي السُّطُوحِ وَغَيْرِهَاMlango Wa Chumba Cha Ghorofa Na Chumba Cha Juu, Kinachochungulia Na Kisichochungulia, Juu Ya Mapaa Na Kwingineko

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ ـ رضي الله عنهما ـ قَالَ أَشْرَفَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم عَلَى أُطُمٍ مِنْ آطَامِ الْمَدِينَةِ ثُمَّ قَالَ " هَلْ تَرَوْنَ مَا أَرَى إِنِّي أَرَى مَوَاقِعَ الْفِتَنِ خِلاَلَ بُيُوتِكُمْ كَمَوَاقِعِ الْقَطْرِ ".

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Muhammad, amesema: Ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitazama kutoka juu ya ngome moja miongoni mwa ngome (aatwaam) za Madiynah, kisha akasema: “Je, mnaona ninachokiona? Hakika mimi ninaona mahali fitna zinapoangukia kati ya nyumba zenu kama mahali matone ya mvua yanapoangukia.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
133
Hadiyth
2467

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي ثَوْرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ ـ رضي الله عنهما ـ قَالَ لَمْ أَزَلْ حَرِيصًا عَلَى أَنْ أَسْأَلَ عُمَرَ ـ رضي الله عنه ـ عَنِ الْمَرْأَتَيْنِ مِنْ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم اللَّتَيْنِ قَالَ اللَّهُ لَهُمَا {إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا} فَحَجَجْتُ مَعَهُ فَعَدَلَ وَعَدَلْتُ مَعَهُ بِالإِدَاوَةِ، فَتَبَرَّزَ حَتَّى جَاءَ، فَسَكَبْتُ عَلَى يَدَيْهِ مِنَ الإِدَاوَةِ، فَتَوَضَّأَ فَقُلْتُ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ مَنِ الْمَرْأَتَانِ مِنْ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم اللَّتَانِ قَالَ لَهُمَا {إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ} فَقَالَ وَاعَجَبِي لَكَ يَا ابْنَ عَبَّاسٍ عَائِشَةُ وَحَفْصَةُ، ثُمَّ اسْتَقْبَلَ عُمَرُ الْحَدِيثَ يَسُوقُهُ، فَقَالَ إِنِّي كُنْتُ وَجَارٌ لِي مِنَ الأَنْصَارِ فِي بَنِي أُمَيَّةَ بْنِ زَيْدٍ، وَهْىَ مِنْ عَوَالِي الْمَدِينَةِ، وَكُنَّا نَتَنَاوَبُ النُّزُولَ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم فَيَنْزِلُ يَوْمًا وَأَنْزِلُ يَوْمًا، فَإِذَا نَزَلْتُ جِئْتُهُ مِنْ خَبَرِ ذَلِكَ الْيَوْمِ مِنَ الأَمْرِ وَغَيْرِهِ، وَإِذَا نَزَلَ فَعَلَ مِثْلَهُ، وَكُنَّا مَعْشَرَ قُرَيْشٍ نَغْلِبُ النِّسَاءَ، فَلَمَّا قَدِمْنَا عَلَى الأَنْصَارِ إِذَا هُمْ قَوْمٌ تَغْلِبُهُمْ نِسَاؤُهُمْ، فَطَفِقَ نِسَاؤُنَا يَأْخُذْنَ مِنْ أَدَبِ نِسَاءِ الأَنْصَارِ، فَصِحْتُ عَلَى امْرَأَتِي، فَرَاجَعَتْنِي، فَأَنْكَرْتُ أَنْ تُرَاجِعَنِي، فَقَالَتْ وَلِمَ تُنْكِرُ أَنْ أُرَاجِعَكَ فَوَاللَّهِ إِنَّ أَزْوَاجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم لَيُرَاجِعْنَهُ، وَإِنَّ إِحْدَاهُنَّ لَتَهْجُرُهُ الْيَوْمَ حَتَّى اللَّيْلِ. فَأَفْزَعَنِي، فَقُلْتُ خَابَتْ مَنْ فَعَلَتْ مِنْهُنَّ بِعَظِيمٍ. ثُمَّ جَمَعْتُ عَلَىَّ ثِيَابِي، فَدَخَلْتُ عَلَى حَفْصَةَ فَقُلْتُ أَىْ حَفْصَةُ، أَتُغَاضِبُ إِحْدَاكُنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم الْيَوْمَ حَتَّى اللَّيْلِ فَقَالَتْ نَعَمْ. فَقُلْتُ خَابَتْ وَخَسِرَتْ، أَفَتَأْمَنُ أَنْ يَغْضَبَ اللَّهُ لِغَضَبِ رَسُولِهِ صلى الله عليه وآله وسلم فَتَهْلِكِينَ لاَ تَسْتَكْثِرِي عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم وَلاَ تُرَاجِعِيهِ فِي شَىْءٍ وَلاَ تَهْجُرِيهِ، وَاسْأَلِينِي مَا بَدَا لَكِ، وَلاَ يَغُرَّنَّكِ أَنْ كَانَتْ جَارَتُكِ هِيَ أَوْضَأَ مِنْكِ وَأَحَبَّ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم ـ يُرِيدُ عَائِشَةَ ـ وَكُنَّا تَحَدَّثْنَا أَنَّ غَسَّانَ تُنْعِلُ النِّعَالَ لِغَزْوِنَا، فَنَزَلَ صَاحِبِي يَوْمَ نَوْبَتِهِ فَرَجَعَ عِشَاءً، فَضَرَبَ بَابِي ضَرْبًا شَدِيدًا، وَقَالَ أَنَائِمٌ هُوَ فَفَزِعْتُ فَخَرَجْتُ إِلَيْهِ. وَقَالَ حَدَثَ أَمْرٌ عَظِيمٌ. قُلْتُ مَا هُوَ أَجَاءَتْ غَسَّانُ قَالَ لاَ، بَلْ أَعْظَمُ مِنْهُ وَأَطْوَلُ، طَلَّقَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم نِسَاءَهُ. قَالَ قَدْ خَابَتْ حَفْصَةُ وَخَسِرَتْ، كُنْتُ أَظُنُّ أَنَّ هَذَا يُوشِكُ أَنْ يَكُونَ، فَجَمَعْتُ عَلَىَّ ثِيَابِي، فَصَلَّيْتُ صَلاَةَ الْفَجْرِ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم فَدَخَلَ مَشْرُبَةً لَهُ فَاعْتَزَلَ فِيهَا، فَدَخَلْتُ عَلَى حَفْصَةَ، فَإِذَا هِيَ تَبْكِي. قُلْتُ مَا يُبْكِيكِ أَوَلَمْ أَكُنْ حَذَّرْتُكِ أَطَلَّقَكُنَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَتْ لاَ أَدْرِي هُوَ ذَا فِي الْمَشْرُبَةِ. فَخَرَجْتُ، فَجِئْتُ الْمِنْبَرَ، فَإِذَا حَوْلَهُ رَهْطٌ يَبْكِي بَعْضُهُمْ، فَجَلَسْتُ مَعَهُمْ قَلِيلاً ثُمَّ غَلَبَنِي مَا أَجِدُ، فَجِئْتُ الْمَشْرُبَةَ الَّتِي هُوَ فِيهَا فَقُلْتُ لِغُلاَمٍ لَهُ أَسْوَدَ اسْتَأْذِنْ لِعُمَرَ. فَدَخَلَ، فَكَلَّمَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم ثُمَّ خَرَجَ، فَقَالَ ذَكَرْتُكَ لَهُ، فَصَمَتَ، فَانْصَرَفْتُ حَتَّى جَلَسْتُ مَعَ الرَّهْطِ الَّذِينَ عِنْدَ الْمِنْبَرِ، ثُمَّ غَلَبَنِي مَا أَجِدُ فَجِئْتُ، فَذَكَرَ مِثْلَهُ، فَجَلَسْتُ مَعَ الرَّهْطِ الَّذِينَ عِنْدَ الْمِنْبَرِ، ثُمَّ غَلَبَنِي مَا أَجِدُ فَجِئْتُ الْغُلاَمَ. فَقُلْتُ اسْتَأْذِنْ لِعُمَرَ. فَذَكَرَ مِثْلَهُ، فَلَمَّا وَلَّيْتُ مُنْصَرِفًا، فَإِذَا الْغُلاَمُ يَدْعُونِي قَالَ أَذِنَ لَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم. فَدَخَلْتُ عَلَيْهِ، فَإِذَا هُوَ مُضْطَجِعٌ عَلَى رِمَالِ حَصِيرٍ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ فِرَاشٌ، قَدْ أَثَّرَ الرِّمَالُ بِجَنْبِهِ، مُتَّكِئٌ عَلَى وِسَادَةٍ مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ، فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ، ثُمَّ قُلْتُ وَأَنَا قَائِمٌ طَلَّقْتَ نِسَاءَكَ فَرَفَعَ بَصَرَهُ إِلَىَّ، فَقَالَ " لاَ ". ثُمَّ قُلْتُ ـ وَأَنَا قَائِمٌ أَسْتَأْنِسُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوْ رَأَيْتَنِي، وَكُنَّا مَعْشَرَ قُرَيْشٍ نَغْلِبُ النِّسَاءَ، فَلَمَّا قَدِمْنَا عَلَى قَوْمٍ تَغْلِبُهُمْ نِسَاؤُهُمْ، فَذَكَرَهُ، فَتَبَسَّمَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم، ثُمَّ قُلْتُ لَوْ رَأَيْتَنِي، وَدَخَلْتُ عَلَى حَفْصَةَ، فَقُلْتُ لاَ يَغُرَّنَّكِ أَنْ كَانَتْ جَارَتُكِ هِيَ أَوْضَأَ مِنْكِ وَأَحَبَّ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم ـ يُرِيدُ عَائِشَةَ ـ فَتَبَسَّمَ أُخْرَى، فَجَلَسْتُ حِينَ رَأَيْتُهُ تَبَسَّمَ، ثُمَّ رَفَعْتُ بَصَرِي فِي بَيْتِهِ، فَوَاللَّهِ مَا رَأَيْتُ فِيهِ شَيْئًا يَرُدُّ الْبَصَرَ غَيْرَ أَهَبَةٍ ثَلاَثَةٍ. فَقُلْتُ ادْعُ اللَّهَ فَلْيُوَسِّعْ عَلَى أُمَّتِكَ، فَإِنَّ فَارِسَ وَالرُّومَ وُسِّعَ عَلَيْهِمْ وَأُعْطُوا الدُّنْيَا، وَهُمْ لاَ يَعْبُدُونَ اللَّهَ، وَكَانَ مُتَّكِئًا. فَقَالَ " أَوَفِي شَكٍّ أَنْتَ يَا ابْنَ الْخَطَّابِ أُولَئِكَ قَوْمٌ عُجِّلَتْ لَهُمْ طَيِّبَاتُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ". فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ اسْتَغْفِرْ لِي. فَاعْتَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ الْحَدِيثِ حِينَ أَفْشَتْهُ حَفْصَةُ إِلَى عَائِشَةَ، وَكَانَ قَدْ قَالَ " مَا أَنَا بِدَاخِلٍ عَلَيْهِنَّ شَهْرًا ". مِنْ شِدَّةِ مَوْجَدَتِهِ عَلَيْهِنَّ حِينَ عَاتَبَهُ اللَّهُ. فَلَمَّا مَضَتْ تِسْعٌ وَعِشْرُونَ دَخَلَ عَلَى عَائِشَةَ فَبَدَأَ بِهَا، فَقَالَتْ لَهُ عَائِشَةُ إِنَّكَ أَقْسَمْتَ أَنْ لاَ تَدْخُلَ عَلَيْنَا شَهْرًا، وَإِنَّا أَصْبَحْنَا لِتِسْعٍ وَعِشْرِينَ لَيْلَةً، أَعُدُّهَا عَدًّا. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم " الشَّهْرُ تِسْعٌ وَعِشْرُونَ ". وَكَانَ ذَلِكَ الشَّهْرُ تِسْعٌ وَعِشْرُونَ. قَالَتْ عَائِشَةُ فَأُنْزِلَتْ آيَةُ التَّخْيِيرِ فَبَدَأَ بِي أَوَّلَ امْرَأَةٍ، فَقَالَ " إِنِّي ذَاكِرٌ لَكِ أَمْرًا، وَلاَ عَلَيْكِ أَنْ لاَ تَعْجَلِي حَتَّى تَسْتَأْمِرِي أَبَوَيْكِ ". قَالَتْ قَدْ أَعْلَمُ أَنَّ أَبَوَىَّ لَمْ يَكُونَا يَأْمُرَانِي بِفِرَاقِكَ. ثُمَّ قَالَ " إِنَّ اللَّهَ قَالَ {يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لأَزْوَاجِكَ} إِلَى قَوْلِهِ { عَظِيمًا} ". قُلْتُ أَفِي هَذَا أَسْتَأْمِرُ أَبَوَىَّ فَإِنِّي أُرِيدُ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الآخِرَةَ. ثُمَّ خَيَّرَ نِسَاءَهُ، فَقُلْنَ مِثْلَ مَا قَالَتْ عَائِشَةُ.

Ametusimulia Yahyaa bin Bukayr, amesema: Ametusimulia Al-Layth, kutoka kwa 'Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: Amenijulisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Thawr, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Sikuacha kuwa na hamu ya kumuuliza 'Umar (رضي الله عنه) kuhusu wanawake wawili miongoni mwa wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao Allaah Aliwaambia:

إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا

Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (basi ni kheri kwenu), kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kwa yanayomchukiza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)) [At-Tahriym (66:4)]

Basi nikahiji pamoja naye. Akachepuka (kutoka njiani), nami nikachepuka pamoja naye na idaawah (kiriba kidogo cha maji). Akaenda kujisaidia mpaka akarudi, nikammiminia maji mikononi mwake kutoka katika idaawah, akatawadha. Nikasema: Yaa Amiyrul-Muuminiyn (Kiongozi wa Waumini), ni akina nani wanawake wawili miongoni mwa wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao (Allaah) Aliwaambia:

إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ

Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah

Akasema: Ajabu iliyoje kwako, yaa Ibn 'Abbaas! (Hao ni) 'Aaishah (رضي الله عنها) na Hafswah (رضي الله عنها). Kisha 'Umar (رضي الله عنه) akaielekea Hadiyth (hiyo) akiisimulia, akasema: Hakika mimi nilikuwa, pamoja na jirani yangu mmoja miongoni mwa Answaar, katika Bani Umayyah bin Zayd — nayo ni katika viunga vya juu vya Madiynah — na tulikuwa tukipokezana kuteremka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Yeye huteremka siku moja nami huteremka siku moja. Nikiteremka, humletea habari ya siku hiyo kuhusu amri (ya Wahyi) na mengineyo; na akiteremka yeye, hufanya mfano wa hayo. Na sisi jamii ya Quraysh tulikuwa tukiwashinda wanawake (wetu). Tulipowafikia Answaar, tahamaki wao ni watu wanaoshindwa na wanawake wao. Wanawake wetu wakaanza kuchukua katika adabu za wanawake wa Answaar. Nikampigia kelele mke wangu, akanijibu (akabishana nami); nikachukia kwamba ananijibu. Akasema: Na kwa nini unachukia nikujibu? Wa-Allaahi, hakika wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) humjibu, na hakika mmoja wao humhama leo (mchana wote) mpaka usiku. Jambo hilo likanitia hofu, nikasema: Amekhasirika aliyefanya hivyo miongoni mwao, (amefanya) jambo kubwa. Kisha nikajikusanyia nguo zangu, nikaingia kwa Hafswah (رضي الله عنها), nikasema: Yaa Hafswah, je, mmoja wenu humkasirisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) leo (mchana wote) mpaka usiku? Akasema: Ndiyo. Nikasema: Amekhasirika na amepata hasara! Je, unajiaminisha kwamba Allaah Hatakasirika kwa kukasirika kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), ukaangamia? Usimdai Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mengi, wala usimjibu katika jambo lolote, wala usimhame; na uniombe mimi unachokihitaji. Wala isikudanganye kwamba jirani yako (mke mwenzako) ni mzuri zaidi kuliko wewe na anapendwa zaidi na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) — anamkusudia 'Aaishah (رضي الله عنها). Na tulikuwa tumezungumza kwamba (watu wa) Ghassaan wanawavisha farasi (wao) viatu ili watushambulie. Sahibu yangu akateremka siku ya zamu yake, akarudi usiku, akaupiga mlango wangu mpigo mkali, akasema: Je, amelala yeye? Nikashtuka, nikamtokea. Akasema: Limetokea jambo kubwa. Nikasema: Ni lipi? Je, Ghassaan wamekuja? Akasema: Hapana, bali ni kubwa zaidi kuliko hilo na refu zaidi: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake. ('Umar (رضي الله عنه)) amesema: Hafswah (رضي الله عنها) amekhasirika na amepata hasara! Nilikuwa nikidhani kwamba hili li karibu kutokea. Nikajikusanyia nguo zangu, nikaswali Swalaah ya Alfajiri pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akaingia katika chumba chake cha juu (mashrubah), akajitenga humo. Nikaingia kwa Hafswah (رضي الله عنها), tahamaki analia. Nikasema: Nini kinakuliza? Je, sikuwa nimekutahadharisha? Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki? Akasema: Sijui. Yeye yuko huko katika chumba cha juu. Nikatoka, nikaja kwenye mimbari, tahamaki kuizunguka kuna kikundi cha watu, baadhi yao wanalia. Nikaketi pamoja nao kidogo, kisha yakanishinda (yale) ninayoyahisi, nikaja kwenye chumba cha juu ambacho yeye yumo, nikamwambia kijana wake mmoja mweusi: Muombee 'Umar (رضي الله عنه) idhini. Akaingia, akazungumza na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha akatoka, akasema: Nimekutaja kwake, akanyamaza. Nikaondoka mpaka nikaketi pamoja na kikundi kile kilichokuwa kwenye mimbari. Kisha yakanishinda ninayoyahisi, nikaja; (kijana) akataja mfano wa hayo. Nikaketi pamoja na kikundi kilichokuwa kwenye mimbari. Kisha yakanishinda ninayoyahisi, nikamjia yule kijana, nikasema: Muombee 'Umar (رضي الله عنه) idhini. Akataja mfano wa hayo. Nilipogeuka kuondoka, tahamaki kijana ananiita, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekupa idhini. Nikaingia kwake, tahamaki amejilaza ubavu juu ya mkeka uliofumwa kwa ukindu, hakuna tandiko baina yake na (mkeka) huo; mafumo ya mkeka yameacha alama ubavuni mwake, naye ameegemea mto wa ngozi uliojazwa nyuzi za mtende. Nikamsalimia, kisha nikasema hali nimesimama: Je, umewataliki wake zako? Akainua macho yake kunitazama, akasema: “Hapana.” Kisha nikasema hali nimesimama, nikitaka kumzoeza (kumliwaza): Yaa Rasula-Allaah, lau ungeliniona! Na sisi jamii ya Quraysh tulikuwa tukiwashinda wanawake; tulipowafikia watu ambao wanawake wao wanawashinda — akataja (habari hiyo). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatabasamu. Kisha nikasema: Lau ungeliniona, nilipoingia kwa Hafswah (رضي الله عنها) nikamwambia: Isikudanganye kwamba jirani yako ni mzuri zaidi kuliko wewe na anapendwa zaidi na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) — anamkusudia 'Aaishah (رضي الله عنها). Akatabasamu mara nyingine. Nikaketi nilipomwona ametabasamu. Kisha nikainua macho yangu (nikatazama) katika nyumba yake; Wa-Allaahi, sikuona humo kitu chochote cha kurudisha macho (cha kutazamwa) isipokuwa ngozi tatu (zisizotengenezwa). Nikasema: Mwombe Allaah Awapanulie Ummah wako (riziki), kwani Faaris (Waajemi) na Ruwm (Warumi) wamepanuliwa na wamepewa dunia, na hali wao hawamwabudu Allaah. Naye alikuwa ameegemea, akasema: “Je, wewe uko katika shaka, yaa Ibn Al-Khatwtwaab? Hao ni watu waliotangulizwa vizuri vyao katika uhai wa dunia.” Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, niombee Maghfirah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijitenga (na wake zake) kwa sababu ya Hadiyth ile, Hafswah (رضي الله عنها) alipoifichua kwa 'Aaishah (رضي الله عنها). Na alikuwa amesema: “Mimi sitaingia kwao mwezi mmoja,” kwa sababu ya ukali wa hasira yake juu yao, Allaah Alipomlaumu. Zilipopita (siku) ishirini na tisa, aliingia kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), akaanza naye. 'Aaishah (رضي الله عنها) akamwambia: Hakika wewe uliapa kwamba hutaingia kwetu mwezi mmoja, na hakika sisi tumeamka (katika siku) ya usiku wa ishirini na tisa, ninauhesabu hesabu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mwezi ni (siku) ishirini na tisa.” Na mwezi ule ulikuwa (siku) ishirini na tisa. 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Ikateremshwa Aayah ya kuwapa hiari (wake zake), akaanza nami, mwanamke wa kwanza, akasema: “Hakika mimi nitakutajia jambo, na si vibaya kwako usifanye haraka mpaka uwashauri wazazi wako wawili.” Amesema: Hakika najua kwamba wazazi wangu wawili hawakuwa wa kuniamrisha kufarikiana nawe. Kisha akasema: Hakika Allaah Amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لأَزْوَاجِكَ

Ee Nabiy! Waambie wake zako [Al-Ahzaab (33:28)]

…mpaka:

عَظِيمًا

adhimu [Al-Ahzaab (33:29)]

Nikasema: Je, katika hili ndio niwashauri wazazi wangu wawili? Kwani hakika mimi namtaka Allaah na Rasuli Wake na Nyumba ya Aakhirah. Kisha akawapa hiari wake zake (wengine), nao wakasema mfano wa alivyosema 'Aaishah (رضي الله عنها).

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
133
Hadiyth
2468

حَدَّثَنَا ابْنُ سَلاَمٍ، حَدَّثَنَا الْفَزَارِيُّ، عَنْ حُمَيْدٍ الطَّوِيلِ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ آلَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم مِنْ نِسَائِهِ شَهْرًا، وَكَانَتِ انْفَكَّتْ قَدَمُهُ فَجَلَسَ فِي عِلِّيَّةٍ لَهُ، فَجَاءَ عُمَرُ، فَقَالَ أَطَلَّقْتَ نِسَاءَكَ قَالَ " لاَ، وَلَكِنِّي آلَيْتُ مِنْهُنَّ شَهْرًا ". فَمَكُثَ تِسْعًا وَعِشْرِينَ، ثُمَّ نَزَلَ، فَدَخَلَ عَلَى نِسَائِهِ.

Ametusimulia Ibn Salaam, amesema: Ametusimulia Al-Fazaariy, kutoka kwa Humayd At-Twawiyl, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliapa kutowaendea wake zake mwezi mmoja, na mguu wake ulikuwa umeteguka, akakaa katika chumba chake cha ghorofa ('illiyyah). 'Umar (رضي الله عنه) akaja, akasema: Je, umewataliki wake zako? Akasema: “Hapana, lakini nimeapa kutowaendea mwezi mmoja.” Akakaa (siku) ishirini na tisa, kisha akashuka, akaingia kwa wake zake.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2469

26-Mlangoباب مَنْ عَقَلَ بَعِيرَهُ عَلَى الْبَلاَطِ أَوْ باب الْمَسْجِدِMlango Wa Aliyemfunga Ngamia Wake Juu Ya Sakafu Ya Mawe (Al-Balaatw) Au Mlangoni Mwa Msikiti

حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، حَدَّثَنَا أَبُو عَقِيلٍ، حَدَّثَنَا أَبُو الْمُتَوَكِّلِ النَّاجِيُّ، قَالَ أَتَيْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضي الله عنهما ـ قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم الْمَسْجِدَ، فَدَخَلْتُ إِلَيْهِ، وَعَقَلْتُ الْجَمَلَ فِي نَاحِيَةِ الْبَلاَطِ فَقُلْتُ هَذَا جَمَلُكَ. فَخَرَجَ فَجَعَلَ يُطِيفُ بِالْجَمَلِ قَالَ " الثَّمَنُ وَالْجَمَلُ لَكَ ".

Ametusimulia Muslim, amesema: Ametusimulia Abuw 'Aqiyl, amesema: Ametusimulia Abul-Mutawakkil An-Naajiy, amesema: Nilimwendea Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), akasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Msikitini, nami nikaingia kwake, na nikamfunga ngamia katika upande mmoja wa al-balaatw (sakafu ya mawe iliyokuwa mbele ya Msikiti). Nikasema: Huyu ni ngamia wako. Akatoka, akaanza kumzunguka ngamia, akasema: “Thamani na ngamia ni vyako.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2470

27-Mlangoباب الْوُقُوفِ وَالْبَوْلِ عِنْدَ سُبَاطَةِ قَوْمٍMlango Wa Kusimama Na Kukojoa Kwenye Jaa La Takataka La Kaumu Fulani

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ حُذَيْفَةَ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ لَقَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم، أَوْ قَالَ لَقَدْ أَتَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم سُبَاطَةَ قَوْمٍ فَبَالَ قَائِمًا.

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه), amesema: Hakika nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) — au amesema: Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alifika kwenye jaa la takataka la kaumu fulani, akakojoa hali amesimama.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2471

28-Mlangoباب مَنْ أَخَذَ الْغُصْنَ وَمَا يُؤْذِي النَّاسَ فِي الطَّرِيقِ فَرَمَى بِهِMlango Wa Aliyeliokota Tawi Na Kinachowaudhi Watu Njiani, Akakitupa

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ سُمَىٍّ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ، وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ فَأَخَذَهُ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ ".

Ametusimulia 'Abdu-Allaah, amesema: Ametujulisha Maalik, kutoka kwa Sumayy, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wakati mtu mmoja anatembea njiani, alikuta tawi la miiba, akaliondoa. Allaah Akamshukuru kwa hilo, Akamghufuria.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2472

29-Mlangoبَابُ إِذَا اخْتَلَفُوا فِي الطَّرِيقِ الْمِيتَاءِ- وَهْيَ الرَّحْبَةُ تَكُونُ بَيْنَ الطَّرِيقِ- ثُمَّ يُرِيدُ أَهْلُهَا الْبُنْيَانُ، فَتُرِكَ مِنْهَا الطَّرِيقُ سَبْعَةَ أَذْرُعٍMlango Wa Wanapotofautiana Kuhusu Njia Ya Wapitaji Wote (Al-Miytaa) — Nayo Ni Uwanja Ulio Katikati Ya Njia — Kisha Wenyewe Wakataka Kujenga, Iachwe Humo Njia Ya Dhiraa Saba

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنِ الزُّبَيْرِ بْنِ خِرِّيتٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ قَضَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم إِذَا تَشَاجَرُوا فِي الطَّرِيقِ بِسَبْعَةِ أَذْرُعٍ.

Ametusimulia Muwsaa bin Ismaa'iyl, amesema: Ametusimulia Jariyr bin Haazim, kutoka kwa Az-Zubayr bin Khirriyt, kutoka kwa 'Ikrimah: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu, (watu) wanapozozana kuhusu njia, (iachwe) dhiraa saba.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2473

30-Mlangoباب النُّهْبَى بِغَيْرِ إِذْنِ صَاحِبِهِMlango Wa Kupora (An-Nuhbaa) Bila Idhini Ya Mwenyewe

حَدَّثَنَا آدَمُ بْنُ أَبِي إِيَاسٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا عَدِيُّ بْنُ ثَابِتٍ، سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ يَزِيدَ الأَنْصَارِيَّ ـ وَهُوَ جَدُّهُ أَبُو أُمِّهِ ـ قَالَ نَهَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم عَنِ النُّهْبَى وَالْمُثْلَةِ.

Ametusimulia Aadam bin Abiy Iyaas, amesema: Ametusimulia Shu'bah, amesema: Ametusimulia 'Adiyy bin Thaabit: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd Al-Answaariy — naye ni babu yake, baba wa mama yake — amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kupora (an-nuhbaa: Kunyakua mali ya watu hadharani bila idhini yao) na kukatakata viungo (al-muthlah).

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2474

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عُفَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنَا عُقَيْلٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم " لاَ يَزْنِي الزَّانِي حِينَ يَزْنِي وَهْوَ مُؤْمِنٌ، وَلاَ يَشْرَبُ الْخَمْرَ حِينَ يَشْرَبُ وَهْوَ مُؤْمِنٌ، وَلاَ يَسْرِقُ حِينَ يَسْرِقُ وَهْوَ مُؤْمِنٌ، وَلاَ يَنْتَهِبُ نُهْبَةً يَرْفَعُ النَّاسُ إِلَيْهِ فِيهَا أَبْصَارَهُمْ حِينَ يَنْتَهِبُهَا وَهْوَ مُؤْمِنٌ ". وَعَنْ سَعِيدٍ وَأَبِي سَلَمَةَ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم مِثْلَهُ إِلاَّ النُّهْبَةَ.

Ametusimulia Sa'iyd bin 'Ufayr, amesema: Amenisimulia Al-Layth, amesema: Ametusimulia 'Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mzinifu hazini wakati anapozini naye ni Muumini; wala (mtu) hanywi khamr (pombe) wakati anapoinywa naye ni Muumini; wala haibi wakati anapoiba naye ni Muumini; wala hapori nyara ambayo watu wanamwinulia macho yao humo wakati anapoipora naye ni Muumini.” Na kutoka kwa Sa'iyd na Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake, isipokuwa (hawakutaja) uporaji.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
135
Hadiyth
2475

31-Mlangoباب كَسْرِ الصَّلِيبِ وَقَتْلِ الْخِنْزِيرِMlango Wa Kuvunja Msalaba Na Kumuua Nguruwe

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنَا الزُّهْرِيُّ، قَالَ أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيَّبِ، سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم قَالَ " لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَنْزِلَ فِيكُمُ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الْخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الْجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ الْمَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ ".

Ametusimulia 'Aliy bin 'Abdi-Allaah, amesema: Ametusimulia Sufyaan, amesema: Ametusimulia Az-Zuhriy, amesema: Amenijulisha Sa'iyd bin Al-Musayyib kwamba alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: “Qiyaamah haitasimama mpaka ateremke kwenu Ibn Maryam akiwa hakimu muadilifu; atavunja msalaba, na atamuua nguruwe, na ataiondoa jizyah (kodi ya wasiokuwa Waislamu), na mali itafurika mpaka asipatikane yeyote wa kuikubali.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2476

32-Mlangoبَابُ هَلْ تُكْسَرُ الدِّنَانُ الَّتِي فِيهَا الْخَمْرُ أَوْ تُخَرَّقُ الزِّقَاقُMlango Wa Je, Yavunjwe Mapipa Ya Udongo Yenye Khamr Ndani Yake, Au Vipasuliwe Viriba?

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ الضَّحَّاكُ بْنُ مَخْلَدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي عُبَيْدٍ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ الأَكْوَعِ ـ رضي الله عنه ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم رَأَى نِيرَانًا تُوقَدُ يَوْمَ خَيْبَرَ. قَالَ " عَلَى مَا تُوقَدُ هَذِهِ النِّيرَانُ ". قَالُوا عَلَى الْحُمُرِ الإِنْسِيَّةِ. قَالَ " اكْسِرُوهَا، وَأَهْرِقُوهَا ". قَالُوا أَلاَ نُهْرِيقُهَا وَنَغْسِلُهَا قَالَ " اغْسِلُوا ". قَالَ أَبُو عَبْد اللَّهِ كَانَ ابْنُ أَبِي أُوَيْسٍ يَقُولُ الْحُمُرِ الْأَنْسِيَّةِ بِنَصْبِ الْأَلِفِ وَالنُّونِ

Ametusimulia Abuw 'Aaswim Adh-Dhwahhaak bin Makhlad, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy 'Ubayd, kutoka kwa Salamah bin Al-Akwa' (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliona mioto ikiwashwa siku ya Khaybar. Akasema: “Mioto hii inawashwa kwa ajili ya nini?” Wakasema: Kwa ajili ya (nyama ya) punda wa kufugwa. Akasema: “Vivunjeni (vyungu hivyo), na mwageni (vilivyomo).” Wakasema: Je, tusimwage (vilivyomo) na tuvioshe? Akasema: “Osheni.” Abuw 'Abdi-Allaah amesema: Ibn Abiy Uways alikuwa akisema: الْحُمُرِ الْأَنْسِيَّةِ, kwa fat-hah juu ya alif na nuun.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2477

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم مَكَّةَ، وَحَوْلَ الْكَعْبَةِ ثَلاَثُمِائَةٍ وَسِتُّونَ نُصُبًا فَجَعَلَ يَطْعَنُهَا بِعُودٍ فِي يَدِهِ وَجَعَلَ يَقُولُ {جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ} الآيَةَ.

Ametusimulia 'Aliy bin 'Abdi-Allaah, amesema: Ametusimulia Sufyaan, amesema: Ametusimulia Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Abuw Ma'mar, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Makkah, na kuizunguka Al-Ka'bah kulikuwa na masanamu (nuswub) mia tatu na sitini. Akaanza kuyadunga kwa kijiti kilichokuwa mkononi mwake, na akaanza kusema:

جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ

Haki imekuja, na ubatili umetoweka [Al-Israa (17:81)]

mpaka mwisho wa Aayah.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2478

حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ عِيَاضٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ الْقَاسِمِ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضي الله عنها ـ أَنَّهَا كَانَتِ اتَّخَذَتْ عَلَى سَهْوَةٍ لَهَا سِتْرًا فِيهِ تَمَاثِيلُ، فَهَتَكَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وآله وسلم، فَاتَّخَذَتْ مِنْهُ نُمْرُقَتَيْنِ، فَكَانَتَا فِي الْبَيْتِ يَجْلِسُ عَلَيْهِمَا.

Ametusimulia Ibraahiym bin Al-Mundhir, amesema: Ametusimulia Anas bin 'Iyaadhw, kutoka kwa 'Ubaydi-Allaah, kutoka kwa 'Abdir-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake Al-Qaasim, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwamba yeye alikuwa ameweka juu ya sahwah (kibanda kidogo cha kuwekea vitu) yake pazia lenye picha (za viumbe). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akalichana. Akatengeneza kutokana nalo mito miwili ya kuegemea, ikawa ndani ya nyumba, (Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)) akiikalia.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2479

33-Mlangoباب مَنْ قَاتَلَ دُونَ مَالِهِMlango Wa Aliyepigana Kuilinda Mali Yake

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ ـ هُوَ ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ ـ قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو الأَسْوَدِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو ـ رضي الله عنهما ـ قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ " مَنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ ".

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, amesema: Ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb — amesema: Amenisimulia Abul-Aswad, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa 'Abdi-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Aliyeuawa akiilinda mali yake, basi yeye ni shahidi.”

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2480

34-Mlangoباب إِذَا كَسَرَ قَصْعَةً أَوْ شَيْئًا لِغَيْرِهِMlango Wa Akivunja Bakuli Au Kitu Cha Mtu Mwingine

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ حُمَيْدٍ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضي الله عنه ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وآله وسلم كَانَ عِنْدَ بَعْضِ نِسَائِهِ، فَأَرْسَلَتْ إِحْدَى أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِينَ مَعَ خَادِمٍ بِقَصْعَةٍ فِيهَا طَعَامٌ فَضَرَبَتْ بِيَدِهَا، فَكَسَرَتِ الْقَصْعَةَ، فَضَمَّهَا، وَجَعَلَ فِيهَا الطَّعَامَ وَقَالَ " كُلُوا ". وَحَبَسَ الرَّسُولَ وَالْقَصْعَةَ حَتَّى فَرَغُوا، فَدَفَعَ الْقَصْعَةَ الصَّحِيحَةَ وَحَبَسَ الْمَكْسُورَةَ. وَقَالَ ابْنُ أَبِي مَرْيَمَ أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ أَيُّوبَ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، حَدَّثَنَا أَنَسٌ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وآله وسلم.

Ametusimulia Musaddad, amesema: Ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa kwa mmoja wa wake zake. Mmoja wa Mama wa Waumini akatuma pamoja na mtumishi bakuli lenye chakula. (Mke ambaye alikuwa kwake) akapiga (mkono wa mtumishi) kwa mkono wake, akalivunja bakuli. Akaliunganisha, akatia ndani yake chakula, na akasema: “Kuleni.” Na akamzuia mjumbe na bakuli mpaka walipomaliza (kula); akatoa bakuli zima, na akalizuia lililovunjika. Na Ibn Abiy Maryam amesema: Ametujulisha Yahyaa bin Ayyuwb, amesema: Ametusimulia Humayd, amesema: Ametusimulia Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
136
Hadiyth
2481

35-Mlangoباب إِذَا هَدَمَ حَائِطًا فَلْيَبْنِ مِثْلَهُMlango Wa Akibomoa Ukuta, Basi Na Ajenge Mfano Wake

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضي الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم " كَانَ رَجُلٌ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ، يُقَالُ لَهُ جُرَيْجٌ، يُصَلِّي، فَجَاءَتْهُ أُمُّهُ فَدَعَتْهُ، فَأَبَى أَنْ يُجِيبَهَا، فَقَالَ أُجِيبُهَا أَوْ أُصَلِّي ثُمَّ أَتَتْهُ، فَقَالَتِ اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى تُرِيَهُ الْمُومِسَاتِ. وَكَانَ جُرَيْجٌ فِي صَوْمَعَتِهِ، فَقَالَتِ امْرَأَةٌ لأَفْتِنَنَّ جُرَيْجًا. فَتَعَرَّضَتْ لَهُ فَكَلَّمَتْهُ فَأَبَى، فَأَتَتْ رَاعِيًا، فَأَمْكَنَتْهُ مِنْ نَفْسِهَا فَوَلَدَتْ غُلاَمًا، فَقَالَتْ هُوَ مِنْ جُرَيْجٍ. فَأَتَوْهُ، وَكَسَرُوا صَوْمَعَتَهُ فَأَنْزَلُوهُ وَسَبُّوهُ، فَتَوَضَّأَ وَصَلَّى ثُمَّ أَتَى الْغُلاَمَ، فَقَالَ مَنْ أَبُوكَ يَا غُلاَمُ قَالَ الرَّاعِي. قَالُوا نَبْنِي صَوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَبٍ. قَالَ لاَ إِلاَّ مِنْ طِينٍ ".

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, amesema: Ametusimulia Jariyr bin Haazim, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Palikuwa na mtu mmoja katika Bani Israaiyl akiitwa Jurayj, alikuwa akiswali. Mama yake akamjia, akamwita; akakataa kumwitikia, akasema: Nimwitikie au niswali? Kisha (mama yake) akamjia (tena), akasema:

اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى تُرِيَهُ الْمُومِسَاتِ

Yaa Allaah, Usimfishe mpaka Umwonyeshe makahaba

Na Jurayj alikuwa katika nyumba yake ya ibaada (swawma'ah). Mwanamke mmoja akasema: Hakika nitamtia Jurayj katika fitna. Akajitokeza kwake, akazungumza naye, akakataa. Akamwendea mchungaji, akamwachia nafsi yake (akazini naye), akazaa mtoto wa kiume, akasema: Ni wa Jurayj. Wakamwendea, wakaivunja nyumba yake ya ibaada, wakamteremsha, na wakamtukana. Akatawadha, akaswali, kisha akamwendea yule mtoto, akasema: Yaa mtoto, baba yako ni nani? Akasema: Ni mchungaji. Wakasema: Tutaijenga nyumba yako ya ibaada kwa dhahabu. Akasema: Hapana, isipokuwa kwa udongo.

Mjalada
3
Kitabu
46
Ukurasa
137
Hadiyth
2482