Kuku Wa Karai (Pakistani)

Kuku Wa Karai (Pakistani)

Vipimo   

                       

Kuku aliyekatwa vipande vipande

Mafuta - Nusu kikombe cha chai

Nyanya zilizokatwa ndogo ndogo au zilosagwa - 5 - 7 kubwa

Kitunguu saumu (thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi (zipasue katikati) -  3 au 5

Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 2 vijiko vya chai

Gilgilani ya unga (Dania) - 1 kijiko cha chai

Paprika -  1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano ya unga - 2 vijiko vya chai

Chumvi -  kiasi

Kotmiri iliyokatwa ndogondogo - 1 kikombe kimoja

Kasuri methi (majani makavu ya uwatu) 1 kijiko cha supu

Ndimu - 2 vijiko vya supu.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Tia mafuta katika karai yashike moto vizuri.
  2. Tia Thomu na tangawizi kaanga kidogo tu.
  3. Tia nyanya, pilipili mbichi, na bizari zote.
  4. Mtie kuku na mkaange katika masala hayo.
  5. Funika karai na wacha moto wa kiasi, kuku atoe maji yake na  apikike.
  6. Karibu na kuwiva kuku tia kotmiri iliyokatwakatwa, kasuri methi, na ndimu.
  7. Funua karai na endelea kukaanga mpaka awive kuku,  muepue na tayari kuliwa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share