Skip to main content

Imaam Ibn Baaz: Ghiybah (Kusengenya) Ni Haraam Na Katika Al-Kabaair (Madhambi Makubwa)

Ghiybah (Kusengenya) Ni Haraam Na Katika Al-Kabaair (Madhambi Makubwa)

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

Alhidaaya.com

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wamekubaliana ‘Ulamaa wa Kiislaam kuwa Ghiybah (Kusengenya) ni Haraam nayo ni katika Al-Kabaair (madhambi makubwa), na ni sawasawa (dhambi zake) ikiwa kuna dosari katika mtu au bila ya kuweko dosari.”

[Majmuw’ Fataawaa Wa Maqalaat Ash-Shaykh Ibn Baaz (5/421)]