Biskuti Za Cornflakes

 

Biskuti Za Cornflake

 

VIPIMO                                           

 

Unga - 1 Kikombe

Sukari ya kusaga -  3/4 Kikombe

Siagi -  125 gms

Yai  - 1

Baking powder -  1/2 kijiko cha chai

Zabibu kavu -   1/2 kikombe

Cornflakes iliyovunjwa (crushed)  - 2 Vikombe

Vanilla - 1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
  2. Tia baking powder, zabibu na unga na changanya   vizuri.
  3. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
  4. Tengeneza viduara vidogo vidogo.
  5. Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
  6. Pika katika moto wa 350ºF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.  

 

 

Share