Skip to main content

Biskuti Za Tende

Biskuti Za Tende

 VIPIMO


Unga -  4 Vikombe vya chai

Sukari ya laini  (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai

Baking powder -  2 Vijiko vya chai

Mayai  - 2

Siagi au margarine -  1 Kikombe cha chai

Vanilla -1 Kijiko cha chai

Maziwa ya kuchanganyia - kiasi

Tende iliyotolewa koko -  1 Kikombe


ufuta (sasame) kiasi  1/4  kikombe

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine.
  2. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane.
  3. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana.
  4. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika.
  5. Vumbika (bake)  moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive.
  6. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)