Skip to main content

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah - Imaam Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)021-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ya Sharti La Yakini Kutoka Katika Qur-aan Na Sunnah

021-Dalili Ya Sharti La Yakini Kutoka Katika Qur-aan Na Sunnah

Swali:

ما دليل اشتراط اليقين من الكتاب والسنة؟

Ni ipi dalili ya sharti la yakini kutoka katika Qur-aan na Sunnah?

Jibu:

قول الله عز وجل:

Ni Kauli ya Allaah (عز وجل):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا

Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka [Al-Hujuraat (49:15)]

أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿١٥﴾

Hao ndio wakweli. [Al-Hujuraat (49:15)]

وقول النبي صلى الله عليه وسلم:

Na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

«أشهد أن لا إله إلا الله وأني رسول الله، لا يلقى الله بهما عبد [غير] شاك فيهما إلا دخل الجنة»

“Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah. Hatokutana na Allaah mja yeyote kwa (shahada) hizo mbili, [bila ya] kuwa na shaka ndani yake, isipokuwa ataingia Jannah (Peponi).” [Ahmad (3/11-421), Muslim (27), Ibn Mandah (36), Ibn Hibbaan (6530) na Al-Bayhaqiy katika Dalaail An-Nubuwwah (5/229-230) kutoka kwa Abu Hurayrah]

وقال صلى الله عليه وسلم لأبي هريرة:

Na amesema (صلى الله عليه وآله وسلم) kumwambia Abu Hurayrah:

«من لقيت وراء هذا الحائط يشهد أن لا إله إلا الله مستيقناً بها قلبه فبشره بالجنة»

“Yeyote utakayekutana naye nyuma ya ukuta huu, akishuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali moyo wake una yakini nayo, basi mbashirie Jannah (Pepo).” [Muslim (31), Ibn Mandah (88) na Ibn Hibbaan (4543) kutoka kwa Abu Hurayrah]

كلاهما في الصحيح.

Hadiyth zote mbili zimo katika Asw-Swahiyh (Swahiyh Muslim).