|
031-Dalili Ya Swalaah Na Zakaah
Swali:
ما دليل الصلاة والزكاة؟
Ni ipi dalili ya Swalaah na Zakaah?
Jibu:
قال الله تعالى:
Allaah (تعالى) Amesema:
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ
Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao. [At-Tawbah (9:5)]
وقال تعالى:
Na Amesema (تعالى):
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini. [At-Tawbah (9:11)]
وقال تعالى:
Na Amesema (تعالى):
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ
Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. [Al-Bayyinah (98:5)]
الآية وغيرها.
Mpaka mwisho wa Aayah. Na (Aayaat) nyinginezo.