Wali, Maharage Na Kamba Wa Rojo

Wali, Maharage Na Kamba Wa Rojo

 

Vipimo:

Wali:

Mchele - 2 Vikombe

Maji - 3 1/2 Vikombe

Chumvi - kiasi

 

Maharage:

Maharage - 4 Vikombe

Kitunguu - 1 kidogo

Nyanya - 1

Pilipili mbichi / mbuzi (ukipenda) -  2 au 3

Tui la nazi   zito - 2 Vikombe 

Ikiwa maharage makavu, osha na roweka kwa muda wa masaa, kisha uchemshe yaive. Au tumia ya tayari ya kopo.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

  1. Kama kawaida ya kupika wali mweupe
  2. Osha mchele, roweka.
  3. Chemsha maji umimine mchele, tia chumvi.
  4. Funika uive moto mdogo mdogo.
  5. Ukipenda wali wa kuchuja maji, ongeza kiasi cha maji.                                  

Namna ya Kutayarisha na Kupika Maharage:

Tia maharage katika sufuria, uweke kwenye moto.

Tia tui zito.   

Katia katika vitunguu, nyanya, pilipili, tia na chumvi.

Acha yapikike hadi upendavyo kiasi cha tui kubakia katika maharage.

Epua na tayari kuliwa na wali au aina yoyote ya mikate.

 

Kamba:

Fuata maelezo ya utayarishaji na upikaji katika mapishi yafuatayo:

 

Kamba Wa Rojo

Share