Kastadi Ya Tambi
Kastadi Ya Tambi
  
Vipimo
Tambi nyembamba za hudhurungi (brown) - 1/2 pakiti
Maziwa mazito (condensed milk) - 1/2 kikopo
Maziwa ya kawaida - 5 kiasi ya vikombe
Sukari - 1/4 kikombe
Kastadi - 2 vijiko vya supu
Hiliki - 1/4 kijiko cha chai
Zaafarani(roweka katika 1/4 kikombe maji) - 1 kijiko cha chai
Vanilla - 1 kijiko cha chai
Lozi za kukata au njugu za pistachio - 1/2 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Katakata tambi kabisa.
 - Katika sufuria tia maziwa kisha uchanganye na kastadi ukoroge.
 - Eka katika moto, tia maziwa mazito (condensed milk), sukari hiliki, zaafarani na vanilla iache ichemke huku unakoroga bila ya kuachia mkoni ili isifanye madonge.
 - Ukiona imekuwa nzito ongeza maziwa mepesi iwe kama kastadi ya kawaida.
 - Tia tambi uendelee kukoroga usiache mkono, ziache kidogo tu ziive epua na umimine katika bakuli iache ipowe.
 - Mwagia lozi juu yake.
 - Tia kwenye friji ikiwa baridi iko tayari.
 
    
    