Kusoma BismiLLaah Katika Kila Suwrah

SWALI:

Assalaam Alaykum, na kheri ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na fadhila zake Insha'Allah zitushukie sote - Amin. Amma ba'ad:

Je, usomapo quraani, ni kweli kuwa kusema Bismillahi ni Sunna na siyo faradhi? Kwa hiyo tunaweza kuswali na kusoma Quraani bila ya Bismillahi kama kwenye Suratut Tawba, kwa kuwa Bismillahi ni sunna? Naomba mnijibu haraka, Insha'Allah.

Wabilahi Tawfiq, ndugu yenu katika imaan.

 

 


JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Unapoanza kwanza kusoma Qur-aan inakupasa ujikinge na Shaytwaan kwa kusoma al-Isti'aadhah (A'wudhu Billaahi Minash-shaytwaanir-Rajiym). Kwa sababu hivyo ndivyo tulivyoamrishwa:

 

 

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ

((Na ukisoma Qur-aani muombe Allaah Akulinde na Shaytwaan maluuni)) [an-Nahl: 98] 

 

Kujikinga huko unatakiwa usome ikiwa ni mwanzo wa Suwrah au hata katikati ya Suwrah. Na ikiwa mwanzo wa Suwrah basi lazima isomwe na BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym ilivyo katika kila mwanzo wa Suwrah. Isipokuwa Suwratut-Tawbah pekee ambayo haina BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym. Kwa hiyo hakuna hapa chaguo isomwe BismiLLaahi au isisomwe bali Suwrah zote zenye kuanzwa na BismiLLaah zinapaswa kuisoma BismiLLaah.   

 

Ikiwa umeanza katikati ya Suwrah unaweza kusoma Isti'aadhah pekee ukaendelea na Suwrah, au pia unaweza kusoma zote mbili Isti'aadha na BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym. Na pia wakati ukindeleza Surah japokuwa haina katikati BismiLLaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share