Skip to main content

Mchuzi Wa Nyama Ya Kondoo Kwa Bamia

Mchuzi Wa Nyama Ya Kondoo Kwa Bamia

Vipimo

Nyama ya kondoo 2 Lb (Ratili)

Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi    1 Kijiko cha supu

Bamia katakata

Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai

Vitunguu 2

Nyanya iliyokatwa katwa 4

Chumvi kiasi

Garam masala 1 Kijiko cha supu

Pilipili manga ½ Kijiko cha chai

Nyanya ya kopo 3 Vijiko vya supu

Ndimu 1

Mafuta ya kukaangia Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha nyama pamoja na chumvi, thomu na tangawizi, pilipili na kitunguu kwa maji ya kiasi.
  2. Hakikisha nyama itakapowiva ibakie supu yake kidogo.
  3. Katika sufuria weka mafuta yapate moto, kaanga vitunguu mpaka view rangi ya hudhurungi, tia thomu kaanga kidogo tu.
  4. Kisha tia bizari,  na ukaange kidogo, tia nyanya kaanga zilainike halafu tia nyanya ya kopo.
  5. Mimina supu ya nyama, tia bamia ulokatakata, changanya kisha iwache kwenye moto kidogo kuwivisha bamia.
  6. Tia ndimu kisha mimina katika bakuli na itakuwa tayari kuliwa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)