Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

 

Vipimo

 

Unga   300gm

Siagi 225gm

Icing Sugar 60gm

Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) - 225gm

Vanilla – Vijiko 2 vya chai

Yai -1 

Baking Powder ½  kijiko cha chai

Njugu za vipande    ½  kikombe cha chai

Njugu zilizosagwa   ¼  kikombe cha chai

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini
  2. Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri
  3. Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.
  4. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)
  5. Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe
  6. Yayusha chokoleti  tia kwenye bakuli ndogo.
  7. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande  mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.
  8. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Kidokezo:

Njugu aina yoyote upendazo, njugu za kawaida, au jozi (walnut), lozi (almond) au pistachio.

 

 

 

 

Share