Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki (Greek Orzo Salad)

Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki  (Greek Orzo Salad)

Vipimo:

Orzo  (makaroni madogo dogo kama picha) - 2 Vikombe/200gms

Tango - 1

Nyanya - 1

Pilipili Tamu La kijani - 1

Pilipili Tamu La manjano - 1

Pilipili Tamu La jekundu - 1

Pilipili Tamu La orenji (rangi ya orange) - 1

Zaituni za kijani - ½ kikombe

Zaituni nyeusi - ½ kikombe

Kitunguu chekundu - 1

Kitunguu cha majani (spring onions) - 3 miche (bunch)

Parsley (aina ya kotmiri) - 3 miche (bunch)

Jibini ya feta (feta cheese) au jibini nyeupe (cottage cheese) - 200 gms

Oregano - ¼ kijiko

Nanaa(mint leaves) - 2 misongo

Chachadu Ya Saladi (Salad Dressing)

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Siki ya zabibu au yoyote - 2 vijiko vya supu

Mafuta za zaituun (olive oil) - ¼ kikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai

Namna ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Chemsha orzo kama ilivyo maelezo katika paketi yake. Usiivishe kupindukia mpaka uliowekwa zikawa laini sana. Chuja maji utie katika bakuli la saladi.
  2. Katakata tango, nyanya, mapilipili yote ya mboga, kitunguu vipande vidogo vidogo, tia katika bakuli la orzo.
  3. Katakata (chop) parsely na nanaa, vitunguu vya majani tia katika bakuli la orzo.
  4. Tia zaituni zote, oregano, katakata jibini uchanganye vyote pamoja katika bakuli. Funika vizuri
  5. Wakati tayari kuliwa nyunyizia chachadu ya saladi ikiwa tayari kuliwa kwa kitoweo upendacho.

Namna ya kutengeneza Chachadu (Dressing ya saladi)

  1. Changanya vitu vyote katika mashine ya kusagia (blender) usage.
  2. Wakati wa kupakua au karibu na kupakua ndio umimine juu ya saladi na uchanganye vizuri na saladi.

Kidokezo:

Unaweza kufanya nusu yake ikiwa ni watu kidogo.

 

 

 

Share