Saladi Ya Mahindi

Saladi Ya Mahindi

Vipimo

Majani ya saladi (lettuce) - ½ msongo

Kabeji ya Zambarau - ¼

Mahindi - 1 kikombe

Tango - 1

Kitunguu majani (spring onion) - 3

Nyanya - 2

Salsali (salad dressing)

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 chembe

Chumvi - kiasi

Ndimu au siki - 2 jiko vya supu

Mafuta ya zaytuuni - ¼ kikombe

Pilipili ya unga nyekundu - ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha

  1. Katakata majani ya saladi, kabeji, weka katika bakuli.
  2. Menya tango, katakata tia pamoja.
  3. Chemsha mahindi au tumia ya tayari ya kopo, mwaga maji.
  4. Katakata kitunguu majani, nyanya.
  5. Changanya vitu vyote pamoja.
  6. Tayarisha Salsali yake kwa kuchanganya vitu vyote, weka kando hadi wakati wa kula umwagie juu yake na uchanganye vizuri.

 

Share