Pudini Ya Karameli Ya Kutengeneza Mwenyewe (Home Made) Katika Vibakuli
Pudini Ya Karameli Ya Kutengeneza Mwenyewe (Home Made) Katika Vibakuli
   
Vipimo Vya Karameli
Sukari - 1 ½ kikombe
Maji - ¾ kikombe
Namna Ya Kuatayarisha Na Kupika Karameli
- Washa oveni moto wa 150° (350°F).
 - Tia sukari na maji katika kisufuria, weka katika moto mdogo mdogo, koroga hadi sukari iyayuke.
 - Rashia (brush) pembezoni mwa sufuria kuondosha chembechembe za sukari.
 - Ongeza moto na acha ichemke kwa dakika 8-10 au hadi shira igeuke rangi ya ya hudhurungi iliyokoza.
 - Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vya oveni (oven proof) vya saizi ya ¾ (6 oz).
 - Weka kando dakika 5 iache karameli ipoe na itulie.
 
Vipimo Vya Kastadi:
Maziwa - 1 1/3 kikombe (10 fl oz)
Malai (Cream) - 1 ½ kikombe (6fl oz)
Mayai - 4
Kiiniyai (egg yolks) - 8 mayai
Sukari - ¾ kikombe
Vanilla - 3 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Kastadi
- Tia maziwa na malai katika sufuria, weka katika moto mdogo mdogo hadi iwe dafudafu (warm).
 - Tia mayai, na viini vya mayai, sukari na vanilla katika bakuli jengine na upigie kwa mchapo wa mayai (egg whipp) hadi vichanganyike.
 - Mimina polepole katika mchanganyiko wa maziwa huku unakoroga ili iendelee kuchanganyika.
 - Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vilivyokuwa na karameli.
 - Vipange vibakuli katika treya, kisha tia maji kiasi kufikia ¾ ya usawa wa vibakuli.
 - Pika (Bake) katika oveni kwa muda wa dakila 35 - 40 hadi kastadi itulie na iwive.
 - Epua katika treya weka nje kwa muda kisha viweke katika friji zishike baridi.
 
    
8. Pindua katika sahani ikiwa tayari.
Kidokezo:
Unaweza kutia flavour nyingine badala ya vanilla kama ya chungwa, au kahawa n.k.
    
    