Kaimati Aina Ya 2

Kaimati Aina Ya 2

Vipimo

Unga - 2 vikombe vya chai

Hamira - 1 ½ Kijiko cha chai

Samli - 1 Kijiko cha Supu

Maji - 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Shira - 1 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya unga  Hamira, Samli, maji, kisha  vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
  2. Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
  3. Ziepue na zichuje mafuta.
  4. Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia Shira  zikiwa tayari.

Shira:

Sukari - 2 vikombe

Maji - 1 kikombe

Zaafarani - 1 kijiko cha chai

Hiliki - ¼ kijiko cha chai

Arki (rose flavour) - 3-4 matone

Namna Ya Kutayarisha Shira

  1. Roweka zaafarani katika kibakuli kwa maji ya moto kiasi ya vijiko 3 vya supu.
  2. Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito kidogo.
  3. Tia zaafarani, hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati.

 

Share