Sharbati Ya Embe Na Maziwa

Sharbati Ya Embe Na Maziwa

    

 

Vipimo

Maziwa - 6 Vikombe

Sukari -  ½ Kikombe

Embe iliyochujwa nzito - 1 Kikombe  

 

Namna Ya Kutayarisha   

  1. Changanya maziwa, sukari na urojo mzito wa embe kwenye blenda pamoja na vipande vya barafu mpaka litowe povu.
  2. Mimina kwenye jagi tayari kunywewa.
  3. Ukipenda unaweza kutia tone moja la essence ya rose.

Kidokezo:

Ukipenda unaweza kutumia rojo la  embe zito lilokuwa tayari kwenye makopo   (Mango Pulp)

 

 

Share