Skip to main content

Mkate wa Sinia - Mkate Wa Kumimina (Aina Ya 2)

Mkate wa Sinia - Mkate Wa Kumimina (Aina Ya 2)

 

Vipimo

Mchele - 3 vikombe vya chai

Sukari - 2 kikombe cha chai

Hamira - 1 kijiko cha chai

Ute wa yai - 1 yai

Tui la nazi - 4 kikombe cha chai

Hiliki -  kiasi

Mafuta  (ya kupakia treya) - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Roweka mchele kwenye maji usiku kucha.  
  2. Chuja mchele kisha tia kwenye mashine ya kusagia (blender) usage pamoja na hamira, sukari, iliki na tui la nazi. 
  3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
  4. Kisha tia ute wa yai koroga vizuri .
  5. Paka mafuta kwenye treya au sufuria ya kuchomea kisha mimina mchanganyiko wa mchele .
  6. Choma (Bake) kwenye oveni kwa moto wa 350°C kwa dakika 30-45,  kisha weka moto wa juu (grill) kama dakika 5-10 mpaka ubadike rangi kwa juu.
  7. Utoe kisha ukate vipande pande ukishapoa weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.