Supu Ya Nyama Ya Mbuzi, Adesi Na Mchicha

Supu Ya Nyama Ya Mbuzi, Adesi Na Mchicha

Vipimo

Nyama ya mbuzi - 1 kilo

Kitunguu kikubwa - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu

Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai

Mchicha - 2 magi

Chumvi - Kiasi

Viazi - 2

Kidonge cha supu - 1

Adesi (ukipenda) - 1 Kikombe cha chai

Nyanya - 1

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha adesi na chemsha hadi ziive
  2. Katakata kitunguu na nyanya.
  3. Katika sufuria tia nyama na viungo vyote isipikuwa mchicha, adesi na viazi, kisha iache motoni ichemke hadi nyama iive.
  4. Halafu katakata viazi na uvitia katika supu na ziache zichemke hadi ziive.
  5. Kisha mimina adesi na mwishoe mchicha na iache katika moto kwa muda mfupi tu.
  6. Mimina katika bakuli na supu tayari kuliwa.
Share