Buns Tamu Za Ufuta

Buns Tamu Za Ufuta

Vipimo 

 

Unga -  4 Vikombe vya chai

 

Sukari -  4 vijiko vya supu

 

Chumvi - 1 Kijiko cha chai

 

Hamira - 1 Kijiko cha supu

 

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

 

Siagi -  ¼ Kikombe cha chai

 

Maziwa -  1 ½ Vikombe vha chai

 

Yai -  1 Moja

 

Ufuta - Kiasi ya kunyunyizia juu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.
  2. Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika.
  3. Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.
  4. Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi.
  5. Ziache pahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.
  6. Washa oveni moto wa 350°.
  7. Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu.
  8. Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi na kuweka moto wa juu hadi ziive na kugeuka rangi na zitakuwa tayari kuliwa.
Share