Skip to main content

Du’aa Ya Swalaah ya Dhwuhaa Imethibiti?

Du'aa Ya Swalaah Ya Dhwuhaa Imethibiti?

www.alhidaaya.com

SWALI:

Asalam alaykum,

Swali ni hivi, kwenye swala ya dhuha kuna dua maalum inayotakiwa isomwe? naomba msaada wenu.

JIBU:

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Hakuna Du’aa maalumu katika Swalaah hii, bali unaweza kuomba baada ya kuimaliza Du’aa zozote upendazo mwenyewe.

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu Swalaah hiyo:

Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa: Idadi Ya Rakaa Zake, Wakati Wake Na Fadhila Zake

Na Allaah Anajua zaidi