Visheti -1

Visheti Kwa Shira Ya Zaafarani Na Vanilla

 

Vipimo

 

Unga  -  Vikombe 2

Samli au shortening ya mboga  - 2 Vijiko vya supu

Maziwa  ¾ Kikombe

Iliki - Kiasi

Mafuta ya kukarangia    Kiasi

 

Shira

Sukari  - 1 Kikombe

Maji  ¾ Kikombe

Vanila  ½ Kijiko cha chai

Zafarani

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
  2. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya.
  3. Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
  4. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
  5. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.
  6. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
  7. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
  8. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share