Anaona Dhiki Mumewe Kuoa Mke Mwengine

SWALI:

 

mume wag ameoe mke mingine meme sina raha yeye ilikuwa hampendi ame mingiya shingoni kisha aka mowa sasa ame mwacha meme nawona diki kwenye moyo wangu sababu yayeye kwenda kuwowa yaya akisema mogo amisma ekiwa mownamk an kupendha ekiwa hukumowa una thamby unigebu haraka asalamu alakum wrahmuly wabrakato.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mumeo kuoa mke wa pili.

 

Hakika swali lako haliko wazi ni hivyo limekuwa vigumu kufahamika kirahisi.

Kwa kadiri tulivyolifahamu tunajibu, Mwanamme kuoa mke wa pili ni katika shari’ah ikiwa ataweza kumtimizia kila mmoja haki yake.

 

Kwa hiyo, nasaha yetu kwako ni kwako wewe kuwa na subira na kukubali hukumu hiyo kwa makini na utulivu na bila vishindo. Hilo litampatia hisia nyingine ya yeye kutimiza wajibu. Ukiwa utakuwa ni mwenye kuona dhiki jambo hilo linaweza kukuletea wewe matatizo na hata ugonjwa.

 

Muombe Allaah Aliyetukuka Akupe subira ya kuweza kuvumilia hayo na kuingizwa miongoni wa Waumini wa kweli.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share