Quesadilla (Kay-sa-dee-yya) Ya Kuku Na Uyoga (Spanish)

Quesadilla (Kay-sa-dee-yya) Ya Kuku Na Uyoga (Spanish)

Vipimo:

Kuku kidari (bila mifupa) - 4 mapande au takriban 2lb

*Mikate Ya Tortillas - (14-16)

Tangawizi mbichi na thomu(galic) ilosagwa - kijiko cha supu

Nyanya/tungule - 2

Vitunguu - 2

Pilipili boga la kijani au rangi nyingineyo - 1

Uyoga - 5

Jibini ya cheddar/marble (cheese) - 500gm

Samli - 3 vijiko vya supu

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kisia

*Salsa

Malai machungu (sour cream – ukipenda)   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Katakata (chop) nyanya/tungule, vitunguu, pilipili boga, uyoga weka kando.
 2. Kuna (shred) jibini weka kando.
 3. Chemsha kuku kwa maji kidogo tu pamoja na chumvi, pilipili mang, tangawizi na thomu ilsogawa.
 4. Akishaiva na kukauka maji, epua akipoa katakata vipande vidogodogo (shred or chop)
 5. Katika bakuli, changanya kuku pamoja na nyanya, kitunguu, pilipili boga na uyoga ulokatakata.
 6. Weka kikaangio (frying pan) katika moto wa kiasi paka samli kidogo.
 7. Katika sahani kubwa, weka mkate mmoja wa Tortilla, tia mchanganyiko wa kuku kiasi vijiko 2 vya supu.
 8. Nyunyizia jibini ilokunwa kisha funika kwa mkate mwingine wa Tortilla.
 9. Hamisha mkate wa Tortilla weka kwenda kikaangio kisha fanya kama kuukaanga kama unavyopika chapati na kugeuza upande wa pili pia hadi uwe rangi ya dhahabu-brauni (golden-brown).
 10. Epua weka katika sahani. Kisha kata vipande size upendavyo.
 11. Kula motomoto kwa kutolea na salsa ukipenda au malai machungu (sour cream) utakayoiweka katika kibakuli kidogo.

Kidokezo: 

Tortilla (Mikate ya ki-Spanish) inauzwa tayari madukani.

 

                      

 

Salsa inauzwa tayari au tengeneza mwenyewe sosi yoyote upendayo. Lakini ukipenda unaweza kuila quesadilla bila ya sosi kwani pia tamu mno!

 

Share