Skip to main content

Juisi Ya Mapera Na Karakara/Pasheni (Passion Fruit)

Juisi Ya Mapera Na Karakara/Pasheni

Vipimo

Mapera 5

Karakara/Pasheni (Passion fruit) 9

Sukari kiasi

Maji kiasi

Namna Ya Kutaarisha

  1. Osha na katakata mapera kisha tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage kwa maji kiasi kisha yachuje .
  2. Kata karakara/pasheni toa nyama yake kisha saga katika blender kwa  maji kiasi .
  3. Changanya pamoja na juisi ya mapera na tia sukari kiasi kadiri upendavyo ikiwa tayari