Skip to main content

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah - Imaam Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)011-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Shariy‘ah Ambayo Allaah Ameamrisha Isifuatwe Dini Ila Kwayo

011-Shariy‘ah Ambayo Allaah Ameamrisha Isifuatwe Dini Ila Kwayo

Swali:

ما هو الشرع الذي أمر الله تعالى أن لا يدان إلا به؟

Ni ipi Shariy‘ah ambayo Allaah (تعالى) Ameamrisha kwamba isifuatwe dini ila kwayo?

Jibu:

هي الحنيفية ملة إبراهيم عليه السلام، قال الله تبارك وتعالى:

Ni Al-Hanifiyyah (Dini ya Tawhiyd iliyojiengua na shirki), mila ya Ibraahiym (عليه السلام). Allaah (تبارك وتعالى) Amesema:

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. [Aal-‘Imraan (3:19)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا

Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende [Aal-‘Imraan (3:83)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ

Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake usafihi? [Al-Baqarah (2:130)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-‘Imraan (3:85)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

Je, wanao washirika waliowaamuru dini ambayo Allaah Hakuitolea idhini? [Ash-Shuwraa (42:21)]

وغيرها من الآيات.

Na Aayaat nyinginezo.