Skip to main content

Kitaab At-Tawhiyd (Word Doc) Chapisho La 2 Kimehaririwa 1438H (2017M)56-Kitaab At-Tawhiyd: Kisiombwe Chochote Kwa Wajihi Wa Allaah Isipokuwa Jannah

Mlango Wa 56

بَابٌ لا يُسْأَلُ بِوَجْهِ اَللَّهِ إِلاَّ الْجَنَّةُ

Kisiombwe Chochote Kwa Wajihi Wa Allaah Isipokuwa Jannah


عَنْ جَابِرٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ يُسْأَلُ بِوَجْهِ اَللَّهِ إِلاَّ الْجَنَّةُ))  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kisiombwe chochote kwa Wajihi wa Allaah isipokuwa Jannah)) [Abuu Daawuwd]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1-Makatazo ya kuomba kitu kwa Wajihi wa Allaah (سبحانه وتعالى) isipokuwa Jannah ambayo jambo kuu kabisa. 

2-Kuthibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana Wajihi.