Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

 

Vipimo   

 

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

 

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

 

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa  kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

 1. Changanya viungo vyote upake katika samaki.
 2. Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
 3. Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
 4. Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

 1. Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
 2. Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
 3. Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
 4. Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
 5. Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
 6. Tia chumvi ukoroge  funika upike kama pilau.
 7. Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

 

Share