Imaam Ibn Rajab: Ramadhwaan: Kuomba Al-‘Afwu Kwa Allaah Laylatul-Qadr Na Kusameheana

 

Kuomba Al-‘Afwu Kwa Allaah Laylatul-Qadr  Na Kusameheana

 

 Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Al-‘Afuww (Mwingi wa Kusamehe) ni katika Majina ya Allaah (Ta’aalaa) Naye Hayachukulii makosa ya waja Wake.  Yeye Ndiye Anayeyafuta makosa yao. Anapenda Kusamehe na kwa hiyo Anapenda kuwasamehe waja Wake. 

 

Basi hali kadhaalika Hupenda kwamba waja Wake wasameheane. Basi pindi wanaposameheana, Yeye Hupeleka msamaha Wake juu yao. Na Anapenda msamaha Wake juu yao zaidi kuliko adhabu Yake.

 

 

[Latwaaif Wal-Ma’aarif, uk. 279]

 

 

Share