Skip to main content

Imaam Al-Albaaniy: Haikuthibiti Kuwa Malaika Anayetoa Roho Anaitwa Izraaiyl

 Haikuthibiti Kuwa Malaika Anayetoa Roho Anaitwa Izraaiyl

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Je, ni sahihi kusema jina la Malaika anayetoa roho kuwa anaitwa Izraaiyl?

JIBU:

Hakuna chochote kilicho sahihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kumwita Malaika anayetoa roho kuwa ni Izraaiyl.

[Fataawaa Imaam Al-Albaaniy – Madiynah Wal-Imaaraat]

Tanbihi:

Lilothibiti katika Qur-aan ni kwamba Malaika anayetoa roho ametajwa kama ni Malakul-Mawt (Malaika wa kutoa roho) katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾

“Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa.”  [As-Sajdah: 11]

Lakini haimaanishi kuwa ndio jina lake bali ametajwa hivyo kama ni sifa ya kitendo hicho cha kutoa roho.

Na Allaah Anajua zaidi