Skip to main content

Fataawaa: Twawaaf Na Sa'y10-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Amefanya Twawaaful-Widaa'i Kisha Hakuweza Kuondoka Makkah Wakati Huo

Amefanya Twawaaful-Widaa'i Kisha Hakuweza Kuondoka Makkah Wakati Huo

Al-Lajnah Ad-Daaimah

www.alhidaaya.com

SWALI:

Mtu amefanya Hajj, alipomaliza kafanya twawaaful-widaa'i usiku lakini akashindwa kuondoka Makkah baada ya twawaaf, hivyo akabakia Makkah hadi asubuhi kisha akasafiri. Nini hukmu ya yake?

JIBU:

Shariy’ah inavyopasa ni kuwa twawaaful-widaa'i iwe pindi mtu anapokuwa tayari kuondoka Makkah pale pale kutokana na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Abbaas: "Watu waliamrishwa kuwa kitendo chao cha mwisho (kabla ya kuondoka Makkah) kiwe ni twawaaf katika Ka'abah, isipokuwa kwa wanawake wenye hedhi". [Al-Bukhaariy na Muslim].

Hivyo ikiwa alifanya twawaaf kwa niyyah ya kuondoka usiku kisha akazuilika hadi asubuhi, basi hakuna ubaya In Shaa Allaah. Akiweza kurudia twawaaful-widaa'i kabla ya kuondoka ni bora zaidi.

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 [Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk.84]