Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Kuvaa Dhahabu Katika Sherehe Na Mikusanyiko Ya Furaha

Mwanamke Kuvaa Dhahabu Katika Sherehe Na Mikusanyiko Ya Furaha

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Je inaruhusika kwangu kuvaa dhahabu katika sherehe na mikusanyiko ya furaha?

JIBU:

Anaruhusiwa mwanamke kuvaa dhahabu katika sherehe na mikusanyiko ya furaha madamu tu wanaume wasiokuwa mahaarim wake hawataona, na kwamba walioko naye ni wanawake tu au ni wanaume ambao ni mahaarim wake.

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Swali Namba 5757, Uk 202, Mj 11]