Skip to main content

Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Wa Akili Na Dini

 Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufu Katika Akili  Na Dini

Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

Amesema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah):   

Kutamka niyyah ni upungufu katika akili na  Dini. 

Ama katika Dini kwa sababu ni bid’ah, na katika akili ni kwa sababu ni sawa na ambaye anataka kula chakula husema: “Nanuia kuweka mkono wangu katika chombo hiki kwa kutaka nichote humo tonge la chakula niweke mdomoni mwangu kisha nimeze ili nishibe.”

Basi huu ni ujinga na upumbavu.

[Al-Fataawaa Al-Kubraa (2/213)]