Skip to main content

Vitabu Vya Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي بِنِعْمَتِهِ تَتِمُّ الصَّالِحَاتُ

Himdi Anastahiki Allaah, Ambaye kwa Neema Yake mema hutimia.

Kwa Fadhila na Tawfiyq ya Allaah (سبحانه وتعالى), Alhidaaya.com inawaletea Vitabu vya Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Kiarabu chenye tashkiyl pamoja na tarjama yake ya Kiswahili. 

Sunnah ni chemchemi ya pili ya Dini baada ya Qur-aan Tukufu, nayo ndiyo inayoibainisha Qur-aan. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl (16:44)]

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

«نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا حَدِيثًا فَحَفِظَهُ حَتَّى يُبَلِّغَهُ غَيْرَهُ»

"Allaah Amnawirishe mtu aliyesikia kutoka kwetu Hadiyth, akaihifadhi mpaka akaifikisha kwa mwingine."

[Abuw Daawuwd, At-Tirmidhiy]

Vitabu hivi vimepangwa kwa Vitabu vya Maudhui na Milango yake. Hivyo Mwanafunzi, Mwalimu na kila Muislamu anaweza kufika kwa wepesi kwenye Hadiyth anayoitafuta.

Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Aijaalie kazi hii iwe kwa ajili ya Wajihi Wake Mtukufu, na iwe yenye manufaa makubwa kwa wasomaji wake katika masomo yao, katika 'ibaada zao na katika maisha yao. Aijaalie iwe nzito katika Mizani zetu za hasanaat (mema) Siku ya Qiyaamah. Na Atujaalie sote tuwe miongoni mwa wanaoifuata Sunnah ya Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa 'ilmu na kwa vitendo.

آمِينَ

Bonyeza Hapa Kusoma Vitabu Vya Hadiyth