SWALI:
Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhaana waala Taala, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu.
Je kufanya sherehe kama kusoma maulidi wakati wa ndoa ni halali?
Natanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu Subhaana wa Taala na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukurani kwa swali lako kuhusu kufanya maulidi katika sherehe za ndoa.
Ukisoma katika mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) utaona kuwa hakuna uzushi wa kusoma Mawlid ndani ya ndoa, na yote yanayohusiana na ndoa utayapata ndani ya vitabu hivi viwili muhimu sana katika mas-ala hayo:
Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (Aadabu Az-Zafaaf Fiy As-Sunnat Al-Mutwahharah)
Kusoma Maulidi Kwenye Harusi Badala Kupiga Ngoma Inafaa?
Sherehe Za Harusi Zina Maasi Ya Mchanganyiko, Uzushi Wa Maulidi, Nyimbo Na Kujifakharisha
Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa
Yanayompasa Bwana Harusi Na Bibi Harusi Siku Ya kufunga Ndoa
Na Allaah Anajua zaidi