Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 06-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Damu Inayotoka Puani Inabatilisha Swawm?

06-Damu Inayotoka Puani Inabatilisha Swawm?

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Damu kidogo sana kama vile tone likitoka kwa mwanamke mchana wa Ramadhwaan na damu hii ikaendelea Ramadhwaan nzima ilhali anafunga, Je, Swawm yake itasihi?

JIBU:

Naam. Swawm yake itasihi. Ama tone hili au alama hii si kitu bali ni kama jasho tu, imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amesema: “Kwa hakika nukta au tone hili ni kama vile Riaaf al-anfu sio hedhi. Hivi imetajwa kutoka kwake (Radhwiya Allaahu 'anhu).

Maana ya Riaaf al-anf: Ni damu inayotoka puani.