Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 11-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Wenye Hedhi Na Nifaas Wanaruhusiwa Kula Mchana Wa Ramadhwaan

11-Wenye Hedhi Na Nifaas Wanaruhusiwa Kula Mchana Wa Ramadhwaan

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Je Mwenye hedhi na Nifasi wanaruhusiwa kula mchana wa Ramadhwaan?

JIBU:

Naam. Wanaruhusiwa kula mchana wa Ramadhwaan lakini ni vyema iwe kwa siri na haswa kama kuna kijana katika nyumba kwa sababu huenda likamtatiza (akataka kufungulia  Swawm).