Skip to main content

Fataawaa: Udhwhiyyah (Kuchinja)02-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe

Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Atakayenunua kichinjwa na kumchunga kisha akapata maradhi au kuvunjika mguu wake je, huchinjwa?

JIBU:

Atakayeainisha kichinjwa na kusema: “Hiki ndicho kichinjwa changu huwa ndio kichinjwa.”

a-Akipatwa na maradhi au kuvunjika na ikiwa wewe ndiye uliyesababisha basi hatochinjwa na yapasa kununua mbadala wake au kilicho bora zaidi.

b-Na ikiwa wewe hukusababisha basi atafaa.

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/99)]